Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 22, 2014

Mshale wa Kifo wa Aisha Bui kutua sokoni Jumatatu


Kava la filamu mpya ya Aisha Bui iitwayo Mshale wa Kifo
http://2.bp.blogspot.com/-4RNtqAw9bTI/U9UMKgE0utI/AAAAAAAAKaI/90DPEawIuD0/s1600/10482228_800152790017429_125002049025336857_n.jpg
Aisha Bui katika pozi
FILAMU mpya ya muigizaji nyota wa filamu nchini, Aisha Fat'hi 'Aisha Bui' iitwayo 'Mshale wa Kifo' inatarajiwa kuingia sokoni siku ya Jumatatu, huku mwanadada huyo akitamba kuwa kazi hiyo ni mwanzo wa uhondo kutoka kampuni yake ya Bad Girl Film's.
Akizungumza na MICHARAZO, Aisha Bui alisema filamu hiyo aliyoigiza na wakali kama Mzee Chilo, Gabo wa Zagamba na wengine itaingia sokoni Agosti 25, huku kampuni yake ya bad Girl ikijipanga kuandaa kazi nyingine kali zaidi na hiyo.
Aisha Bui, alisema japo filamu hiyo ni kazi yake ya kwanza kuiandaa, lakini kwa jinsi ilivyoandaliwa kwa umakini mkubwa ni wazi mashabiki watajua ujio wake mpya siyo wa kubahatisha.
"Naiachia filamu yangu Jumatatu, nawaomba mashabiki waniunge mkono kwa kununua nakala halisi, ili kuiwezesha kampuni ya Bad Girl kuendelea kuwapa uhondo zaidi, kuna makubwa yapo njiani kutoka kwangu," alitamba Aisha Bui.
Nyota huyo aliyecheza filamu mbalimbali ikiwamo ya Saturday Morning, Better Days, Not Without My Son, Continous Love, Revenge of Love, Mirathi, Pain of Love, Crazy Love na The Second Wife, alisema ndani ya filamu hiyo mpya inasimulia kisa cha mfanyabiashara wa dawa za kulevya ambaye anamlazimisha askari Polisi kumsaidia kupitisha mzigo wake.
Hata hivyo kazi haiwi rahisi na kuibua kashkash kwa binti wa askari huyo Myrine nafasi iliyochezwa na Aisha kufanywa kama chambo.
"Ni simulizi linalosisimua na kutia simanzi na bahati nzuri walioiigiza kuanzia mimi mwenyewe, Gabo, Mzee Chilo na wengine tumeitendea haki," alisema Aisha.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...