Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, August 20, 2014

MABONDIA MOHAMED MATUMLA NA NASSIBU RAMADHANI KUZIDUNDA TENA SEPTEMBA 27 FRIENDS CORNER MANZESE

Bondia Mohamed Matumla kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli 

Na Mwandishi Wetu

 MABONDIA Nassibu Ramadhani pamoja na Mohamed Matumla wameingia makubaliano ya kuzipiga kwa mara ya pili siku ya septemba 27 katika ukumbi wa

friends corner hotel manzese Dar es salaam

akizungumzia mpambano huo mratibu wake Yassin Abdallah 'Ostadhi' amesema mabondia hawo wamekubaliana na kusaini mkataba wa kuzipiga siku hiyo

ambapo mabondia hawo walikutana mara ya kwanza na bondia Mohamed Matumla alimshinda kwa point Nassibu Ramadhani hivyo kuufanya mchezo huu kuwa mgumu zaidi kwa Matumla kuendeleza kipigo au Ramadhani kurudisha kisasi

 katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano ya utangulizi

 bondia Issa omari atamkabili juma fundi.kg 53 raundi nane. na Sadiq momba vs Tasha mjuaji kg 59 raundi nane. wakati Juma mustafa atamkabili Bakari dunda kg 61 raundi sita. huku kina dada Lulu  Kayage akipambana na fatma yazidu.kg 51 raundi nne.

siku hiyo pia kutakuwa na huuzwaji wa 
DVD ambazo zinatoa mwanga kwa mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa mbali mbali Duniani.

Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama Manny Paquaio,Floyd Maywether,Amir Khani, Mohamed Ali ,Mike Tayson na wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi Duniani
kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...