Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, August 12, 2014

Jennifer Mgendi akaribia kumtoa Mama MkweMUIMBAJI nyota wa Nyimbo za Injili nchini ambaye pia ni muigizaji wa filamu, Jennifer Mgendi anatarajia kuiachia mtaani filamu yake mpya iitwayo 'Mama Mkwe' aliowashirikisha wakali wenzake wa muziki wa injili, Bahati Bukuku na Christina Matai.
Akizungumza na MICHARAZO Jennifer alisema filamu hiyo ipo njiani kuachiwa baada ya kukamilika kuhaririwa na kuwataka mashabiki wake wajiandae kuipokea.
Jennifer anayetamba na albamu ya 'Hongera Yesu', alisema filamu hiyo inayozungumzia mkasa wa mama mkwe anayelazimisha mwanae wa kiume kumzalia mjukuu ameigiza na wasanii kama Senga,Bi Esther, Christine Matai, Husna Chobis, yeye (Jennifer)  na wengine.
"Filamu yangu mpya ya 'Mama Mkwe' bado kidogo kabla ya kuachiwa mtaani ikiwa imechezwa na mimi mwenyewe, Bahati (Bukuku) Christine Matai, Senga, Bi Esther, Mussa Banzi na wakali wengine. Siyo ya kuikosa kwa jinsi ilivyo," alisema Jennifer.
Kabla ya filamu hiyo, Jennifer amewahi kutamba na filamu kadhaa kama 'Chai ya Moto', 'Joto la Roho', 'Teke la Mama', na 'Pigo la Faraja'.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...