Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, October 4, 2014

MABONDIA KUZIPIGA JUMAPILI UWANJA WA MKWAKWANI TANGA

Bondia Francis Miyeyusho kushoto akitunishiana misuli naEmilio Norfat ambao watazipiga kesho jumapili

October

5 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga mpambano wa raundi nane  Picha na www.superdboxingcoach,blogspot.com
 MABONDIA mbalimbali kuzipiga siku ya jumapili kwa ajili ya mpambano wa ubingwa ambapo bondia kutoka mkoa wa Tanga Tanzania Alen Kamote 'Rasta'' atazipiga na Osgood Kayuni wa Malawi kugombania ubingwa wa Dunia wa UBO kg 61 hiyo ndio siku ya kufurahia wakazi wa tanga mpamano huo pia uatasindikizwa na mapambano mengine

ambapo bondia wa Dar es salaam Thomas Mashali atavaana na bondia kutoka Moshi Allibaba Ramadhani kugombania ubingwa wa Africa wa UBO kg 72 pia siku hiyo kutakuwa na mpambano mwingine  mkali kati ya bondia namba moja kwa ubora katika uzito wake featherweight  Fransic Miyayusho atakaezipiga na Emilio Norfat ambaye nae ni namba mbili katika uzito huo

mipambano hiyo iliyoandaliwa jijini Tanga na promota mkongwe nchini Ally Mwazoa ambaye kwa hivi sasa analeta burudani ya masumbwi nchini kupitia Mwanzoa Promotionsiku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika


mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...