Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, December 23, 2014

WAZIRI TIBAIJUKA OUT KWA FEDHA ZA ESCROW, AFUTWA KAZI NA RAIS KIKWETE


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akizungumza wakati alipokuwa akilihutubiua Taifa katiuka mkutano wake na Wazee uliofanyika jioni hii kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Katika Hotuba yake Mhe. Rais alizungumzia suala la sakata la fedha za Escrow na kutaja mapendekezo na maamuzi ya Kamati maalum ya Bunge la Jamhuri kuhusu suala hilo na kutangaza rasmi kumfuta kazi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, kutokana na kuhusishwa moja kwa moja na upokeaji wa fedha hizo.

Mapema wiki iliyopita. Prof. Tibaijuka aliitishja mkutano na wanahabari na kutangaza rasmi dhamira yake ya kutojiuzulu katika wadhfa wake huo kwa kile alichodai kutohusika na moja kwa moja na suala hilo, huku akijitetea kuwa fedha hizo zilitumwa kwake kwa ajili ya msaada wa shule.

Baada ya Mhe. Rais kutangaza maamuzi hayo ya kumfuta kazi Prof Tibaijuka, ukumbi huo uliripuka kwa shangwe na vigeregere vya kumpongea Rais kwa maamuzi hayo, huku kwa upande wa Prof. Mhongo, ikielezwa kuwa suala lake bado linafanyiwa kazi na uchunguzi utakapokamilika basi nalo litatolewa maamuzi.
 Rais Jakaya Kikwete, akiendelea kuzungumza na Wazee, ukumbini hapo (kushoto) ni Makamu wa Rais, Dkt. Mhammed Gharib Bilal, na (katikati) ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza, kumsikiliza mhe. Rais.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza, kumsikiliza mhe. Rais.
Baadhi ya mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi, waliohudhuria.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza, kumsikiliza mhe. Rais.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza, kumsikiliza mhe. Rais.
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa, akitafakari hotiba ya Rais Jakaya.
Viongozi wa dini waliohudhuria 
Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan, wakati akiondoka ukumbini hapo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...