Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 8, 2012

BENDI YA EXTRA BONGO YAZINDUA RASMI UKUMBI WAKE WA NEW WHITE HOUSE KIMARA KOROGWE



Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, akiimba jukwaani mbele ya mashabiki lukuki wa bendi hiyo ndani ya ukumbi wao mpya New White House, utakaojulikana kwa jina la 'Bongo Resort Kimara Korogwe' wakati wa onyesho maalum la uzinduzi wa ukumbi huo lililofanyika jana. Extra Bongo  walizindua ukumbi huo mpya wa New White House a.k.a Bongo resort uliopo kimara Korogwe, ambapo uzinduzi huo ulisindikizwa na kundi la bendi ya Taarabu ya Coast Modern Taarab, iliyo chini ya Omary Tego na Maua Tego, na wasanii wa muziki wa kizazi kipya kama, Tunda Man, Sheta na kundi maarufu la BAIKOKO kutoka Mkoa wa Tanga.
Rogert Hegga. 'Katapila' akiimba jukwaani wakati wa onyesho hilo katika ukumbi wao mpya uliopo Kimara Korogwe Dar es salaam.

Mnenguaji mahiri wa Extra bongo akishambulia jukwaa.
Wanenguaji wa kiume wa bendi hiyo, Danger Boy (kushoto) na Super Nyamwela, wakishambulia jukwaa.
Jembe la Extra Bongo Banza Stone A.K.A Makaveli, akipagawisha wapenzi wao ndani ya White Inn Kimara Korogwe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...