Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 8, 2012

Watanzania Kusherekea Saba Saba na CD " BONGO TAMBARARE





 Nyimbo za Supu ya Mawe na Uhuru wa Habari Kutinga
Redioni

Wakati tukiwa katika shamra shamra ya sikuu ya Saba Saba, watanzania tunafurahia sikukuu hii kwa kupata burudani ya raha ya nyimbo
mpya zilizopo katika CD "Bongo Tambarare" kutoka kwa bendi maarufu ya
muziki wa dansi  Ngoma Africa Band aka FFU yenye maskani nchini Ujerumani,

CD hiyo yenye nyimbo tatu  "Bongo Tambarare" , "Supu ya Mawe" na "Uhuru wa Habari"
Inasemekana imeshaanza kupiga hodi katika milango ya vituo mbali mbali vya redio
duniani na hapa nyumbani itasikika wakati wowote kuanzia sasa,hili watanzania wenye
Bongo Tambarare yao wapate raha ya muziki.

CD hiyo yenye nyimbo tatu zilizojaa ujumbe wenye furaha na mafunzo kwa jamii,
kama vile "Supu ya Mawe" ni utunzi na  wake kiongozi wa bendi hiyo
kamanda Ras Makunja wa FFU akiimba kwa kushirikiana na mpiga solo
afande Chris-B.
Watanzania tuipokee CD "Bongo Tambarare" na tufurahie Saba Saba kwa
kupata raha ya "Supu ya Mawe" kutoka kwa Kikosi kazi Ngoma Africa aka FFU.
unaweza kusikiliza pia at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...