Mchezaji wa timu ya Yanga Juma Abdul akijaribu kunyang'anya mpira
kutoka kwa beki wa timu ya Atletico Henry Mbazumutima kwenye mchezo wa
pili wa fungua dimba katika michuano ya kombe la Kagame inayoandaliwa na
shirikisho la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki CECAFA
inayofanyika jijini Dar es salaam Tanzania, Mpira umekiwasha na timu ya
Yanga imeambulia kipigo cha magoli 2-0 yaliyofungwa na mchezji Didier
Kavumbagu wa Atletico
Wachezaji wa timu za Yanga ya Tanzania na Atletico ya Burundi
wakichuana vikali katika mchezo wao uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa
jioni ya leo.
Mashabiki wa mpira wakiwa kwenye uwanja wa Taifa kwa ajili ya
kushuhudia pambano la michuano ya Kagame kwenye uwanja wa Taifa kati ya
Yanga ya Tanzania na Atletico ya Burundi
Mashabiki wa timu
ya Yanga wakiwa wamefurika uwanjani kwa ajili ya kushuhudia mchezo kati
ya timu yao na timu ya Atleticokutoka Burundi. PICHA ZADI TEMBELEA http://www.fullshangweblog.com/
No comments:
Post a Comment