Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 9, 2012

BENKI YA KIISLAM YA WATU WA ZANZIBAR (PBZ) WAFUTURU NA MAKAMU WA RAIS DK. BILAL


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongazana  na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana Agosti 8, 2012 kuhudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki hiyo na kufutari pamoja na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) akiwaongoza baadhi ya Viongozi wa dini na Serikali ‘kujisevia’ futari wakati wa  hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na kufuturu  pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Bilal na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa katika hafla hiyo, jana Agosti 8, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...