Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 9, 2012

Hatimaye Mahalu na mwenzake hawana hatia

Bi Grace Martine (kushoto) na Balozi Mahalu wakiwa wamezingukwa na waandishi wa habari wakiwa hata kwenye kizmba cha mahakama hawajatoka mara baada ya hukumu hiyo wakitaka kujua namna walivyopokea hukumu hiyo, ambapo Mahalu na Mwenzake wakidaiwa kufanya ufisadi kwenye ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kwa kununua kwa bei iliyochini ya ile iliyopangwa na Serikali.
Mahalu akikumbatiana na mdogowake Miras Rama, mara baada ya hukumu mahakamani hapo.
Punde tu ndugu jamaa na marafiki wakaanza kumtwangia simu na kuwaeleza hivi "ukweli umepatikana na haki imetendeka subiri baadaye tutazungumza 'Ahsante' " alisema mahalu.
Hapa Mahalu (katikati)akizungumza na wakiliwake Mabere Marando (kulia) pamoja na jamaa wengine.
Waandishi nao walikua hawatosheki kila wakati walimtaka aongelee kwa undani namna kesi hiyo ilivyokwenda lakini aliishia kusema "haki imetendeka na nimefurahi kwa hukumu hii".
Pongezi zikaendelea zaidi nje kwenye viwanja vya mahakama hiyo Kisutu jijini Dar es salaam.
Grace Martine akimuangalia kwa furaha wakili wao aliyesimamia kesi hiyo Mabre Marando kulia.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...