Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, August 4, 2012

BINGWA MICHUANO YA BANCABC SUPER 8 KUPATA MIL 40/-


Mkurugenzi Mtendaji wa Muunganiko wa Makampuni ya BancABC, Douglas Munatsi (kulia) akimkabidhi kombe Makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani kwa ajili ya mashindano ya BancABC SUP8R wakati wa uzinduzi rasmi uliofanyika Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

Bingwa wa michuano ya BancABC Super 8 inayoanza keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) katika miji ya Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza na Arusha atapata sh. milioni 40 wakati makamu bingwa sh. milioni 20. Pia timu mbili zitakazoishia hatua ya nusu fainali kila moja itapata sh. milioni 15 wakati zilizobaki kila moja itapata sh. milioni 5.

Timu zimepangwa katika makundi mawili ya A na B. Kundi A lina timu za Simba (mabingwa wa Tanzania Bara), Jamhuri, Zimamoto na Mtende zote za Zanzibar. Kundi ni Super Falcon (mabingwa wa Zanzibar), Azam, Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro zote za Tanzania Bara.

Mechi za ufunguzi keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) ni Simba vs Jamhuri (Dar es Salaam), Zimamoto vs Mtende (Mwanza), Mtibwa Sugar vs Polisi Morogoro (Arusha) na Super Falcon vs Azam (Zanzibar). Awali mashindano yalikuwa yaanze Agosti 4 mwaka huu lakini yamesogezwa mbele kwa siku moja.


Hatua ya makundi itamalizika Agosti 12 mwaka huu. Mechi za nusu fainali na fainali zote zitachezwa Dar es Salaam.

Mdhamini bancABC atagharamia usafiri wa ndege kwa timu zote kutoka kituo kimoja hadi kingine, malazi na jezi. Yanga imejitokea kwenye mashindano hayo na nafasi yake imechukuliwa na Mtibwa Sugar ambayo ilishika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...