Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, August 4, 2012

MDAU Melleck achukua fomu UVCCM


Mkuu wa Idara ya Oganizesheni na Siasa UVCCM, Taifa, Sophia Duma (kulia) akimkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Innocent Melleck katika ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Vijana jijini Dar es Salaam.

Na Andrew Chale

KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Umoja wa Vijana wa (UVCCM), Innocent Melleck, amejitosa kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa wa UVCCM Tanzania Bara.
Mellack alichukua fomu hiyo jana kwenye ofisi za makao makuu ya UVCCM jijini Dar es Salaam na kusema kuwa yeye  ni miongoni mwa watoto wa mkulima, hivyo kuchukua fomu na kuwania nafasi hiyo anawakilisha  vijana hao.


“Nimechukua fomu nikiwa miongoni mwa watoto wa mkulima na kuwawakilisha vijana wote wa Tanzania, nitahakikisha narudisha hadhi UVCCM, na pia kuujenga umoja huu kuwa wa hadhi,” alisema.


Aidha, alisema kugombea kwake hajashawishiwa na mtu na wala hana makundi ndani ya umoja huo, kwani anachohitaji  ni kuleta mabadiliko  ya kweli na kuondoa ubinafsi uliojijenga kwa muda mrefu.


Melleck alikabidhiwa fomu hiyo na Mkuu wa Idara ya Oganizesheni na Siasa UVCCM, Taifa, Sophia Duma, ambapo alitakiwa kuirejesha baada ya kuijaza na mwisho wa kurudishwa ni Agosti 6.


Tayari vijana mbalimbali wameshajitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti huku ile ya Mwenyekiti nafasi yake wagombea watatoka Tanzania Visiwani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...