Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, August 4, 2012

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa achukua fomu za kugombea UVCCM -NEC


Naibu katibu mkuu wa UVCCM Zanzibar, Jamal Kasim Ally akimkabithi fomu za kugombea nafasi ya uongozi wa UVCCM-NEC Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Bw Jerry Silaa jana katika ofisi za CCM mkoa mjini magharibi Zanzibar, (ktk) mwenye suti nyeusi ni Bw Abdallah Mwinyi-katibu wa vijana mkoa kusini unguja akishuhudia tukio hilo. UVCCM -NEC imetangaza nafasi zinazogomewa kua ni Mwenyekiti, Mkamu mwenyekiti, Katibu, wajumbe wa baraza kuu na wajumbe wa halmashauri. Hata hivo mstahiki meya wa manispaa ya ilala alipohojiwa hakuweka wazi nafasi gani anayotaka kugombea kwani alikua bado anakusanya maoni na ushauri kutoka watanzania mbalimbali na kujipima mwenyewe ni nafasi ipi itakayo mfaa zaidi ili kuweza kuwatumukia wananchi vema.Tetesi kutoka kwa wadau wake wa karibu zinasema  mstahiki meya anataka kugombea nafasi ya Mwenyekiti UVCCM-NEC.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...