Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, August 7, 2012

TIMU YA MPIRA WA MIGUU TA (TCS) ACADEMY YA MWANZA YAREJEA NA MATAJI KIBAO KUTOKA NCHINI UJERUMANI


 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Street Children Sports Academy TSC ya Mwanza Bw. Mutani Yangwe akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Karume wakati akielezea mafanikio ya timu ya Academy yao waliyoyapata kutoka nchini Ujerumani na kunyakua  mataji mbalimbali na zawadi kemkem. amesema takribani wachezaji saba wamefanikiwa kupata ofa ya kufanya majairibio nje watatu wakihitajika katika timu ya Makabi Haifa ya Israel na wengine wanne wakipata ofa kwenda nchini Sweden ambako watapitia kisha kwenda nchini Ujerumani.
Katikati katika picha ni Altaf Hirani Rais wa kituo hicho na kushoto ni kocha wa kutuo hicho Bw. Rogashian Kaijage
Altaf Hirani Rais wa Taasisi ya Tanzania Street Children Sports Academy TSC ya Mwanza akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ofisi za shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF kulia ni Mkurugenzi wa TCS Mutani Yangwe na kushoto ni Mmoja wa maofisa wa kituo hicho B. Leonard Magomba.
Viongozi wa kituo hicho wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo kutoka TCS Mwanza mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakiwa na mataji yao waliyoijishindia na zawadi mbalimbali.

1 comment:

  1. I don't understand your language, but I see that you're doing an interview for the football team, good luck,

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...