Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, January 10, 2014

ABIRIA WA TRENI WAENDELEA KUTESEKA DODOMA, UONGOZI WA TRL MKOANI DODOMA WAWAKODISHIA MABASI


 
 Abiria waliokwama na treni Dodoma wakisubiri mabasi kwa ajili ya usafiri  wa kuelekea kwenye mikoa ya Morogoro na Dar es saalam ambapo shirika la Reli  limewakodia mabasi kutokana na kushindwa kuendelea na safari kutokana na Mafuriko Gulwe na Godegode wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
 Abiria hao wakiwa hawajui la kufanya kutokana na kukosa chakula katika  stesheni ya reli mkoani Dodoma walipotangaziwa kuanza kusafirishwa kwa mabasi lakini mpaka kufikia leo jioni zaidi ya abiria 900 kati ya 1600 walikuwa bado  hawajapatiwa usafiri huo.

Mfanyakazi wa shirika Reli kituo cha Dodoma akibandika tangazo katika  ubao wa matangazo lililowataka abiria waliokuwa wanaelekea mikoa ya kanda ya ziwa kurudishiwa nauli zao kutokana na usafiri wa treni kusitishwa kwa muda  usiojulikana.
 Askari wa kuzuia Ghasia (FFU) wakiangalia usalama kwa abiria wa treni  waliokwama kutokana na treni kushindwa kuendelea na  safari tangu juzi mara baada ya kufika kituo cha reli mkoani Dodoma kutokana  na mvua iliofunika reli wilayani Mpwapwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...