Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, January 8, 2014

MKUU WA MKOA AMFUKUZA MKANDARASI KATIKA MKOA WAKEIMG_0989
Mkuu wa mkoa wa Rukwa injinia Stella Manyanya akizungumza wakati akikagua jengo hilo la bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Kasanga wilayani Kalambo. Kulia ni mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Sumbawanga Vijijini ndugu Mtapima na katikati ni Mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Kalambo Issa Liyanga.PICHA NA RAMADHANI JUMA-AFISA HABARI WILAYA YA

 IMG_0996
Mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Kalambo Issa Liyanga akimuonesha kitu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa injinia Stella Manyanya alipokagua jengo la bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Kasanga wilayani Kalambo.
PICHA NA RAMADHANI JUMA-AFISA HABARI WILAYA YA KALAMBO
……………………………………………………………………………….
NA RAMADHANI JUMA,
OFISI YA MKURUGENZI-KALAMBO
MKUU wa mkoa wa Rukwa  Mhandisi Stella Manyanya ameziagiza Halmashauri zote Mkoani hapa pamoja na taasisi nyingine za serikali kutotoa kazi yoyote ya ujenzi kwa kampuni ya ujenzi ya ‘Juin Constructions Company Limited ’ kutokana na kampuni hiyo kuonekana  kufanya kazi zake chini ya kiwango.
 Alitoa maamuzi hayo wakati alipokuwa akikagua jengo la bweni la wasichana linalojengwa katika shule ya sekondari ya Kasanga iliyopo kata ya Kasanga wilaya ya Kalambo Mkoani  Rukwa .
Alisema wakandarasi wengi wamekuwa wakiihujumu mikoa ya pembezoni mwa nchi ukiwemo Mkoa wa Rukwa kwa kujenga miradi isiyo na viwango kwa muda mrefu sasa, na kwamba umefika wakati wa kupambana na hali hiyo.
Aliagiza kampuni hiyo  iwekwe kwenye orodha ya makampuni yasiyotakiwa kupewa kazi katika mkoa wa Rukwa mara moja ili iwe fundisho kwa makampuni mengine yanayolipwa fedha za umma kwa kazi zilizo chini ya kwango.
Mbali kutekeleza jengo hilo chini ya kiwango, Mkuu huyo wa Mkoa pia alisema mkandarasi huyo amekuwa hafuati ushauri wa wataalam wa Halmashauri ya Kalambo iliyompa kazi hiyo.
“Mkandarasi huyu hajawahi kupatikana katika eneo la mradi wakati wa ukaguzi hata siku moja..kila mara wakaguzi wakitembelea mradi huu yeye huwa hayupo kwahiyo huyu hatufai katika mkoa wetu” alifafanua.
Kwa upande wake mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Issa Liyanga alisema wamekuwa wakimsimamia mkandarasi huyo katika hatua mbalimbali za ujenzi wa jengo hilo ambapo hata hivyo amekuwa na ushirikiano hafifu katika kuzingatia ushauri unaotolewa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...