Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 27, 2014

ASKARI 96 WA TANAPA WAMALIZA MAFUNZO YA AWALI WAAHIDI KUPAMBANA NA MAJANGIRI‏Mkurugenzi 
mkuu wa TANAPA Allan kijazi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya  
kuhifadhi maliasili katika chuo cha wanyama pori cha Mlele mkoani katavi 
ambao hawapo pichani hapo juzi katika chuo cha wanyama pori cha mlele  
ambapo wahitimu 96 walihitimu mafunzo ya awali ya wahifadhi wa  
rasilimali za nchi na aliwataka wafanye kazi kwa uadilifu mkubwa ili  
waweze kupambana na kutokomeza ujangiri na kuvunja mitandao ya majangiri 
ya ndani ya nchi na nje ya nchi.

 Askari 
wa hifadhi ya  mbuga ya wanyama (TANAPA)  wakiwa wamesimama
wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA  ambaye hayuko pichani wakati  
akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika  
chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali  
za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu
 

 Askari wa hifadhi ya  mbuga ya wanyama 
(TANAPA) wakiwa wamekaa wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA ALLAN  
KIJAZI ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao  
waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa  
wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu  
hao wafanye kazi kwa uaminifu. 
 Picha na Katavi yetu Blog

*********************
Na   Walter Mguluchuma wa Katavi yetu Blog. Mpanda Katavi


 Jumla ya  
Askari 96 wa  Shirika  la Hifadhi la Taifa  la Wanyama Pori (TANAPA) wametimu    mafunzo  
ya miezi   mitatu  katika  
chuo     kipya   cha wanyama  
pori   cha Mlele  kilichopo   
Mkoa  wa Katavi  na kutoa  
kiapo cha utii  mbele ya Mkurugenzi 
mkuu  wa TANAPA Allan Kijazi


Askari hao  wa TANAPA walimaliza  mafunzo  
hayo  hapo juzi  kwenye chuo 
hicho   cha  wanyama Pori  
cha Mlele  akiwa ni  mafunzo ya 
kwanza  hapa  nchini 
kwa TANAPA  kutoa  mafunzo kama hayo kwa Askari wa wanyama pori 
kupatiwa mafunzo hayo  kabla ya 
kuanza  kazi 
Katika  Risala yao ya 
wahitimu wa mafunzo hayo  ya 
kulinda maliasili  iliyosomwa  na Bruno  
Mbunda  walieleza kuwa 
wamejifundisha  mbinu mbalimbali za 
kulinda   rasilimali za Taifa  kwa Vitendo   
na nadharia


Waliyataja baadhi 
ya mafunzo waliyoyapata kuwa ni namna ya kufanya doria , kukamata  waharifu  
kumpekua  mharifu  na kutotumia  
nguvu  sana  katika kukamata  mharifu    
pamoja  na  pia wamejifundisha namna ya kutumia silaha


Walieleza  katika kipindi hicho cha  mafunzo  
 wahitimi   hao walifanikiwa kukamata  waharifu  
hamsini  wakati  wakifanya  
doria  katika maeneo mbambali ya 
Mbuga ya  Katavi  na kwenye mapori ya akiba ya Rukwa  Lwafi


Wahitimu hao 
walieleza kuwa  mafunzo hayo 
yaliwashirikisha  Askari  99 
lakini  watatu kati yao 
wameshindwa  kuhitimu  zikiwemo 
sababu  mbambali  kama  
utoro na utovu  wa nidhamu   hari ambayo ilfanya wahitimu  waliomaliza kubaki  96 ambapo kati yao mwanamke  ni mmoja 
na wanaume ni  95


Kwa upande wake 
mkuu wamapori ya akiba  ya  Rukwa Lwafi 
Joseph Mbung’ombe alimweleza mkurugenzi mkuu wa TANAPA kuwa chuo hicho 
kinakabiliwa na changamoto mbalimbali 
Alizitaja 
changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa mawasiliano  
na  ubovu wa miundo  mbinu ya barabara  na  
upungufu  wa  magari pamoja  
idadi ndogo ya washiriki  wa
mafunzo kwa wanawake na ufinyu  wa bajeti


Nae  Mkurugenzi  wa Hifadhi  
na Ikolojia  Martini  Loibook  alieleza kuwa mafunzo hayo walioyapata 
yanaumuhimu  sana  hasa kutokana na changamoto  zinazoikabili nchi  yetu  
inayokabiliwa na wimbi la ujangili


Pia Mkurugenzi 
wa  utumishi   na utawalla   
wa TANAPA  Witnes Shoo  aliwataka wahitimu hao  kufanya kazi  
kwa uaminifu  kwa kujituma  na 
wawe na didamu  na  wasiwe na tabia ya kutow a siri za ofisi


Mkurugenzi 
Mkuu   wa TANAPA  Allan Kijazi  
aliwaasa wahitimu hao  wahakikishe 
wanafanya kazi  zao kwa uaminifu 
mkubwa  hasa  katika shughuli zao  katika kupambana kukomesha ujangili 
Aliwataka 
kutojihusisha  na masuala ya ujangiri na 
badal awahakikishe wanafanya kazi za kupambana na mitandao ya ujangiri iliyopo 
ndani ya nchi na nje ya nchi 
Alisema wapo 
baadhi ya watumishi wa TANAPA ambao wamekuwa sio waaminifu hivyo wahitimu hao
wahakikishe wanafanya kazi zao kwa uaminifu pasipo kueubuniwa na mtu yoyote 
yule au watu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...