Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, January 14, 2014

NEWS ALERT.AJALI MBAYA YA BASI LA SHABIBY NA PRINCES MUNAA

Abiria 28 wakiwemo watoto wanne wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wamesafiria la Kampuni ya Shabiby kugongana na Lori tupu la mafuta na kupinduka katika kijiji cha Kisaki umbali wa kilometa 10 kwenye Barabara Kuu ya kutoka Mjini Singida kwenda Dodoma.
Taarifa zilizopatikana kwenye eneo la tukio zimeelezwa kuwa Basi hilo lenye namba T930BUW aina ya Yutong  lililokuwa likiendeshwa na Dereva wake ambaye
amekimbia mara baada ya ajali hiyo linakadiriwa kuwa na abiria wapatao 48 lilipata ajali hiyo jana saa 6:50 mchana wakati lilipojaribu kulipita lori hilo upande wa kulia .
Taarifa hizo ambazo pia zimethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida zinasema kuwa kitendo hicho kilisababisha kuligonga Lori hilo RAA 496N aina ya MECEDES BENZ lililokuwa likitokea Mjini Kigali nchini Rwanda kwenda Dar es Salaam likiwa na dereva wake Barimana Benjamini (37) na kuanguka upande wa kulia wa Barabara na kujeruhi abiria wake .Habari picha kwa hisani ya superfeoblog.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...