Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, January 14, 2014

RAIS KIKWETE MGENI RASMI KONGAMANO LA WASANII IJUMAA


Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Twalib 'Teacher' 
(kushoto)
 
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa kongamano la umoja na mshikamano linalofanyika Januari 17 (Ijumaa) kwenye viwanja vya hoteli ya Lamada ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Caasim Taalib alisema madhumuni ya kongamano hilo ni kuhamasisha umoja kati ya wasanii ili kujenga uwezo na nguvu ya kumaliza matatizo yao ya kiuchumi.
Alisema wasanii, waandishi, wa habari na Vijana wanashindwa kumaliza matatizo yao ya kiuchumi bila kuombaomba au kusubiri misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali.
"Wasanii inatubidi tujifunze kujitegemea na tuache kusubiri wafadhili au serikali ituchangie hata kwa matibabu na katika mazishi yetu" alisema Taalib.

Katika kongamano hilo Shiwata itazingua mpango maalum ambao utawezesha wasanii kupata misaada ya fedha za kutengeneza filamu,kurekodi muziki,kuwezesha timu na vikundi mbalimbali kununua vifaa vya ichezona kuwapatia nauli ya usafiri ndani na nje ya nchi kwa shughuli za michezo na sanaa.

Katika Mpango huo Shiwata pia itatoa fedha kwa mrithi wa msaniii kamaatakufa, akiugua au kulazwa kwa siku tatu katika hospitali zinazotambuliwa na Serikali.

Alisema Shiwata pia itatoia misada kwa wasanii wanaotaka kuoa au kuolewa ambako kila mwanachama atachangia sh. 1,000 kwa ajili ya kugharamikia mazishi ya msanii kununua sanduku n usafiri.

Alisema Shiwata itakusanya zaidi ya sh. Mil.7 kutoka kwa wanachama 7,000 na wasanii watajiunga kwa sh. 20,000 ambazo zinaweza kulipwa kwa awamu tatu kutokana na uwezo wa msanii.
Sjiwata ina ekari 300 za makazi katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga ambapo hivi sasa kuna nyumba 40 zilizojengwa kwa nguvu ya wasanii wenyewe na ekari 500 za kilimo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...