Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, January 23, 2014

VODACOM YAWASOGEZEA HUDUMA WAKAZI WA KINONDONI
Mkuu Wa Idara ya Mauzo ya rejareja wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(Katikati) akishirikiana na Msimamizi wa Duka jipya la Vodacom Kinondoni Donart Alwatani kukata utepe kuashiria kuanza rasmi kwa huduma kwenye duka hilo jipya lililopo eneo la Kinondoni Manyanya Dar es salaam. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Duka hilo litakuwa likitoa huduma kwa siku saba za wiki ikiwemo siku za sikukuu.

Mkuu wa Idara ya Mauzo ya rejareja wa Vodacom Tanzania,Bi.Upendo Richard (wa pili kushoto) akiwawekea Shampeni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim(wa tatu kushoto) na Msimamizi wa Duka jipya la Vodacom lililopo Kinondoni Manyanaya Jijini Dar es salaam Donard Alwatani ikiwa ni ishara ya kulitakia mafanikio duka hilo mara baada ya kuzinduliwa rasmi. Anaeshuhudia ni Meneja Uhusiano kwa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(katikati) akiwa kwenye furaha baada ya kufungua Shampeni kuashiria kuanza rasmi kwa huduma katika duka jipya la kampuni yake lilipo Kinondoni Manyanya Dar es salaam. Kutoka kulia ni Msimamizi wa duka hilo Donart Alwatani, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Mkuu wa Idara ya Mauzo ya rejareja wa Vodacom Upendo Richard na Meneja katika idara hiyo Elihuruma Ngowi.

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (wa kwanza kushoto) akitaniana jambo na Mkuu wa Idara ya Mauzo ya rejareja wa kampuni hiyo Upendo Richard huku wakiwashuhudia Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Msimamizi wa duka jipya la kampuni hiyo lililopo Kinondoni Manyanya jijini Dar es salaam wanavyogida kinywaji cha Shampeni ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa duka hilo.

Hili ndilo Duka jipya la Vodacom lililopo Kinondoni Manyanya Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...