Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, December 17, 2014

ZANZI YAZINDUA RADHA NYINGINE MBILI MPYA CHOCOLATE NA CAPPUCCINO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Desemba 17, 2014


KUZINDULIWA KWA LADHA NYINGINE MBILI ZA KINYWAJI CHA ZANZI CREAM LIQUEUR - CHOCOLATE NA CAPPUCCINO

Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited wazalishaji wa bidhaa bora zaidi za vinywaji vikali na mvinyo  hapa nchini, leo inazindua  ladha mbili nyingine za Zanzi Cream Liqueur. Ladha hizi ni Zanzi Chocolate na Zanzi Cappuccino.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa, alisema ana uhakika ladha hizi mbili  za Zanzi Chocolate na Cappuccino zitapendwa na wengi kwani utafiti ulifanyika wa muda mrefu kubaini ni ladha zipi zitafurahiwa na watu wengi.  Vile vile Zanzi Chocolate na Cappuccino zimetengenezwa kwa kuzingatia ubora na viwango vya Kimataifa katika kuzalisha wa bidha za Cream Liqueur.


Naye Meneja Bidhaa wa TDL, Warda Kimaro alisema, “kauli mbiu ya Zanzi Cream Liqueur toka kuzinduliwa 2012 ilikuwa ‘Fursa ya Kujiliwaza’. Sasa tunawapa wateja wetu fursa nyingine mbili za Kujiliwaza msimu huu wa sikukuu na Zanzi Chocolate na Cappuccino.” Kimaro anawasihi watanzania kujaribu ladha hizo mbili kwani ni za kipekee kwenye jamii ya cream liqueur hapa nchini.
Kinywaji cha Zanzi Cream Liqueur kilizinduliwa 2012 na Tanzania Distilleries Ltd katika chupa zenye ujazo wa 750ml na Pakiti zenye ujazo wa 100ml. June 2013, chupa za ujazo wa 200ml nazo pia zilizinduliwa na kuingizwa sokoni. August 2014, Zanzi Cream Liqueur ilipata tuzo ya kimataifa ya ‘Double Gold Award’ huko New York Marekani kutokana na ubora wake. Mafanikio ya Zanzi Cream Liqueur toka ilipozinduliwa ndio yamehamasisha TDL kuzindua ladha ya Zanzi Chocolate na Cappuccino.

TDL inawatakia wateja wake wote kheri ya Christmas na Mwaka Mpya na kuwasihi washereke na kujiliwaza na Zanzi Chocolate na Zanzi Cappuccino msimu huu wa sikukuu.

-MWISHO-


Kuhusu SABMiller
SABMiller plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara matano. Bia zake ni pamoja na zile za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini India.
SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya London na Johannesburg.
Mkurugenzi Mtendaji wa TDL , David Mgwassa katikati na Meneja Mauzo wa Kampuni ya Konyagi, Joseph Chibehe na Meneja Bidhaa wa Kampuni hiyo Warda Kimaro wakiwaonesha kijwaji cha zanzi walicho kizindua chenye radha ya chocolet na cappuccino leo

1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...