Hivi majuzi niliskia kuwepo kwa tuzo za waandishi wa habari za
mtandaoni maarufu kama waandishi wa magazeti tando (blogs). Katika Tuzo
hizo ambazo ziliandaliwa kwa vigezo wanavyovijua Vodacom, wametajwa
washindi fulani. Kama mdau wa kawaida katika magazeti tando, miongoni
mwa waasisi wa Bloger wa kwanza kabisa wa Kitanzania naamini kwa sasa
kama nchi hii itakuwa inaendeshwa kishkaji, kirafiki, kima kundi na
ikaachwa bila kukemewa basi siku si nyingi tutapoteza ladha ya
mashindano yanayopima viwango na ubora wa kazi hali itakayofanya nchi
kubakia kuwa ya wababaishaji kila siku.
Eneo hili la magazeti tando niliwahi kulilalamikia
kutokana na kukosekana ubunifu hasa inapotokea habari moja inajaa kila
blog kama ambavyo ipo katika magazeti ya Tanzania. Kwa kuona hili hili
nashangaa blog iliyo na kazi ya kubandika picha za magazeti ya kila siku
ama habari za wasanii walio nje au kuchota mawazo ya watu katika FB na
twitter, au kusubiri taarifa za Maafisa Habari ikaibuka mshindi kwa kuwa
tu eti inaonesha kuwa na wasomaji wengi. Kwamba hamjui kuwa ukiseti
weblog yako ihesabu wanaoitembelea itahesabu bila kujali ni nani
anaingia mara ngapi?
Kwa mantiki hii kigezo cha idadi ya watu si muwli kuonesha kuwa huyu ni mahiri katika kutoa taarifa katika Blog yake.
Natoa
rai, kuwa mliopata nafasi ya kuwa na nguvu katika makampuni msitumie
nafasi hizo vibaya kwa kutaka kuidhinisha udhamini wa blog kwa rafiki
zenu na kisha kupoteza ladha ya ubunifu katika blog. Najua mmefanya hivi
sana katika maeneo kama ya sanaa za urembo na kwingineko lakini
kumbukeni hili limezidi na haliwezi kuvumiliwa! Jamhuri hii ilikuwepo
kabla yenu na hiki mnachojivunia kwa kuwa kimetengenezwa na urithi wa
Baba zenu msitarajie kitabaki kuwa hivi kila siku. Tendeni haki japo
kidogo jamii hii itawaheshimu.
Kwa masikitiko na hasira kidogo nawasilisha!
Bonny Makene Road to PhD.
http://www.fullshangweblog.com/
No comments:
Post a Comment