Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 3, 2014

SIKU YA SHERIA DUNIANI YAFANYIKA MKOANI DODOMA, WALIA NA UPUNGUFU WA MAJAJI



 Wakili  wa Serekali Mfawidhi mkoa wa Dodoma, Angaza  Mwaipopo akifafanua jambo wakati wa sherehe ya siku ya sheria mjini Dodoma leo.
Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Dodoma, Crecensia  Makuru akizangumza jambo mbele ya watendaji na wadau wa mahakama wakati  sherehe za siku ya Sheria zilizofanyika leo.
 Wakili wa kujitegemea Mary Munissi wa mkoani Dodoma  akielezea jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika  leo
 Mahakimu, Mawakili na watendaji wengine wa  mahakama wakifuatila jambo walipokuwa kwenye maadhimisho ya siku ya  sheria yaliyofanyika leo Dodoma.
 Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Dodoma akizungumza jambo na Kaimu mkuu wa mkoa wa Dodoma ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Singida, Mh. Pasiseko Konne mara baada ya kumalizika shughuli za maadhimisho  ya siku ya sheria leo.

Na John Banda, Dodoma
UCHELEWESHWAJI wa kesi nyingi mahakamani katika mahakama ya kanda ya Dodoma kunasababishwa na upungufu mkubwa wa majaji. Hayo yalisemwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Crecencia Makuru leo mjini humo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama kuu.
Alisema kuna upungufu mkubwa wa majaji ambao haulingani na kesi zilizopo hali inayosabisha kuzolotatesha mienendo ya kesi mbalimbali.

Crecencia alisema majaji katika kanda ya Dodoma ni wachache kulingana na kesi zilizopo  ambapo hadi kufikia Desemba 31, 2013 kulikuwa na jumla ya mashauri na 1364 na kuna majaji wawili tu. Alisema ''idadi ya kesi ni kubwa mno kwa majaji wawili hii inachangia kwa kiwango kikubwa kesi kutosikilizwa na kutolewa maamuzi kwa wakati, upo umuhimu wa kuongeza majaji ili kuwe na uwiano wa masharti yaliyopo'',

Aidha alisema Mahakimu ni wachache huku mahakama nyingi za wilaya zina hakimu mmoja mmoja licha  ya kuwa na mashauri mengi na tatizo linakuwa kubwa pindi mahakimu hao wanapougua, kuuguliwa au kwenda likizo. Aliongeza kuwa mahakama nyingi za mwanzo hazina mahakimu wa kudumu, mahakama hizo hutembelewa na mahakimu kutoka vituo vingine hali ambayo husababisha ucheleweshaji wa haki kwani mahakimu hulazimika kusafiri umbali mrefu na wakati mwingine miundombinu huwa ni mibovu..

Jaji  huyo alibainisha kuwa sasa posho za washauri wa mahakama zimeboreshwa kutoka Sh.1,500 hadi kufikia 5,000 kwa kila shauri litakalohitimishwa. Alisema licha ya changamoto mbalimbali zinazoikabili mahakama  kuna mikakati ya kutatua changamoto hizo ikiwemo kuondoa mashauri, kesi zote zenye umri zaidi ya miaka miwili, kuboresha takwimu za mashauri, kesi zilizopo mahakamani, kuboresha na kusimamia masjala pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...