Niyonzima (kulia) na Cannavaro (kati) wakiwa na Chuji (24) |
BENCHI la Ufundi la klabu ya Young Africans limekanusha taarifa kwamba nyota wawili wa timu yao, nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' na Haruna Niyonzima 'Fabregas' walipigana katika mchezo dhidi ya Coastal Union uliochezwa juzi jijini Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa kupitia mtandao wa klabu hiyo wa www.youngafricans.co.tz , umemnukuu Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Charles Boniface Mkwasa 'Master' akisemataarifa hizo hazina ukweli wowote bali ni katika kutaka kuharibu twasira ya timu.
Mkwasa amesema benchi la ufundi wameshangazwa na taarifa hizo baada ya kuziona na kuzisoma leo na kusisitiza walioandika wamefanya hivyo kwa ajili ya maslahi yao tu.
Kila mtu alikuwepo uwanjani na aliweza kushuhudia mchezo huo, hakuna aliyeona Cannavaro na Niyonzima wakipigana katika kipindi chote cha dakika 90 za mchezo, nashikwa wasi wasi na waandishi waliokuwepo uwanjani kama walikua makini kufuatilia mchezo na kuandika kitu tofauti na walichokiona.
"Sheria za soka zipo wazi, mchezaji au wachezaji wapigana ndani ya uwanja mwamuzi anawatoa nje ya uwanja kwa kuwapa kadi nyekundu, sasa tumeshangazwa na taarifa hizo zilioripotiwa leo kuwa kuwa kuna wachezaji wetu walipigana ili wachezaji wote walicheza kwa dakika 90 "alisema Mkwasa.
Nadhani imefika wakati tuisaidie jamii kuelewa uhalisia wa jambo husika liliotokea, kwani kuandika tofauti na kilichotokea kunasababisha jamii kuamini/kuelewa jambo ambalo silo lililotokea.
Katika mchezo wowote wachezaji kuelekezana/kukumbushana majukumu ni jambo la kawaida na ndicho kilichotokea katika mchezo dhidi ya Coastal kati ya Cananavaro na Yondani na Niyonzima na Cannavaro na si kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
"Hata mara baada ya mchezo wachezaji wote walikuwa pamoja na kupeana pole kutokana na ugumu wa mechi, kisha wote kuondoka kuelekea hotelini kupumzika, na sisi kama viongozi hatujaona wachezaji kutofautiana kitu chochote hata kufikia hatua ya kusuruhishwa kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari " aliongeza Mkwasa .
Kuhusu maandalizi ya mchezo wa jumapili Mkwasa amesema vijana wake leo wamefanya mazoezi asubuhi kujiandaa na mchezo huo, na hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja kwani Hamis Kiiza, Hassana Dilunga waliokuwa wagonjwa wameshaungana wenzao kambini na Athuman Idd "Chuji" aliyekua amesimamishwa kurejeshwa kundini.
No comments:
Post a Comment