Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 25, 2012

DIKTETA WA CHEKIBUDI AANZA VEMA SOKONI
Na Elizabeth John
MUIGIZAJI wa filamu nchini, Mohamed Nurdin ‘Chekibudi’ ameonekana kupanda kwa kasi katika soko la sanaa, baada ya kuachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Dikteta’, ambayo imeanza kufanya vizuri sokoni.
 
Filamu hiyo mpya inayoonesha ukandamizaji wa familia, imekamilika na kuingizwa sokoni hivi karibuni, ambapo tayari imeanza kufanya vizuri katika mauzo, hasa katika baadhi ya maeneo ya jijini  Dar es Salaam, ikisambazwa na kampuni ya Steps Entertaiment.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Chekibudi alisema, filamu hiyo ameiandaa ili kuonesha ukandamizaji uliopo ndani ya baadhi ya familia katika maisha ya kila siku, na amefarijika kuona Watanzaania wakiipokea vema sokoni.
 
Alisema baada ya kuangalia hilo, aliamua kuweka wazo lake katika filamu ili kuwafikishia ujumbe watu wengi zaidi na ikawa kama ni moja ya kazi za wasanii kuelimisha na kufundisha jamii.
 
“Unajua unapokuwa msanii unatakiwa kuwa mbunifu katika mambo mengi na ndiyo maana kila kukicha tunaangalia ni jinsi gani tutawakumbusha wenzetu matatizo ambayo yanaepukika,” alisema Chekibudi.
 
Chekibudi alishawahi kufanya vizuri alipokuwa katika kundi la sanaa la ‘Splendid’, na katika filamu hiyo ya ‘Dikteta’ amewashirikisha nyota wengine kama, Cojack, Philipo, Munira Sultan, Snura Mush, Coletha Reymond pamoja na nyota wengine.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...