Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 22, 2012

EDDA SYLIVESTER NDIYE MISS TEMEKE 2012


Redd's Miss Temeke 2012, Edda Sylivester (katikati) akipunga mkono kwa furaha akiwa na washindi wenzake mshindi wa pili Catherine Masumbigana (kushoto) na Flaviana Maeda (kulia) mara baada ya kutangazwa washindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa PTA, jijini Dar es Salaam.
*********************************
Edda ambaye ametokea katika shindano la kitongoji cha Kigamboni ataungana na Flaviana Maeda kutoka Kurasini ambaye amenyakuwa nafasi ya pili na kujichukulia kitita cha shilingi 800,000.

Mrembo Catherine Masumbigana amechukua mshindi wa tatu katika shindano hilo na kujinyakulia kitita cha shilingi 700,000.

Warembo hao watatu wamepata nafasi ya kuingia katika kambi ya Redd's Miss Tanzania ambayo itashirikisha jumla ya warembo 30 ambao watakaa kambini kwa muda wa mwezi mmoja.

Warembo Jesca Haule ambaye alishika nafasi ya nne amejipatia kitita cha shilingi 400,000 na nafasi ya tano ilienda kwa Agnes Gudluck ambae amejipatia shilingi 300,000.

Washindi wote watatu kila mmoja atajipatia nguo ya kutokea jioni sanjari na viatu, vikiwa na thamani ya kila mmoja shilingi 500,000 kutoka katika Duka la kisasa la Mariedo Boutique itatoa gauni la Sh.350,000 na kiatu cha Sh 150,000 

kila mmoja kwa washindi hao watatu wa kwanza watakaoshinda. 
Warembo wengine ambao walishiriki kutoka katika vitongoji vya Kurasini,Kigamboni na Chang'ombe ambao ambao wameambualiwa kifuta jasho cha shilingi 200,000 kila mmoja ni Angela Gasper, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.

Katika shindano hilo washehereshaji walikuwa wasanii wanaong’ara katika luninga, Mpoki wa kundi la Komed Original na Steve Nyerere ambao walionekana kuvunja mbavu za mashabiki waliyoudhulia shindano hilo.

Licha ya kuwepo kwa Mpoki na Steven Nyerere Bendi ya muziki Mashujaa Wanakibega ambao waliweza kutoa burudani ya nguvu chini ya Rais wao Charles Baba.

Taji la Redd's Miss Temeke, linashikiliwa na mrembo Husna Twalib. Warembo wa Miss Temeke wamekuwa wakijifua kwa wiki tatu sasa chini ya ukufunzi wa Leyla Bhanji, ambaye amekuwa akisaidiwa pia na warembo wa miaka ya nyuma wa Miss Temeke akiwemo, Regina Mosha(20020, Hawa Ismail(2003), washiriki wa mwaka jana Joyce Maweda, Mwajabu Juma, Cynthia Kimasha na katika shoo wamekuwa na Dickson Daud kutoka kundi la THT.

Mbali ya Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na City Sports Lounge, Jambo Leo, Mariedo Boutique, Global Publishers, Dodoma Wine, Push Mobile, Mariedo Boutique, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Fredito Entertainment, katejoshy.blogsport.com na 88.4 Cloud's FM. 

Temeke imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo Happiness Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy Baham mwaka 2003 na Genevieve Mpangala. Lakini pia imetoa warembo waliowahi 

kushika nafasi ya pili na tano bora katika Miss Tanzania kama Jokate Mwegelo, Irene Uwoya, Irene Kiwia, Queen David, Cecylia Assey, Sabrina Slim, Miriam Odemba, Ediltruda Kalikawe na Asela Magaka

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...