Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 22, 2012

MANCINI: HAKUNA MWENYE NAMBA YA KUDUMU MAN CITY


MANCHESTER, England
“Kama unataka kufanya vema kwenye mashindano yote unayoshiriki, wachezaji wanapaswa kubadilishwa. Ndicho kitachotokea, kwamba mchezaji muhimu kikosini anaweza kukalia benchi”
KOCHA Roberto Mancini wa Manchester City amewaonya nyota wake na kuwaambia hakuna aliye na namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England.
Mancini amesisitiza kuwa, anaweza kumshusha yeyote kikosini miongoni mwa wakali wake walioigharimu timu mabilioni ya fedha, kama njia kuu ya mabingwa hao wa England kupigania ushindi katika mataji manne wanayowania.
Mancini alisema: “Kama unataka kwenda sawa katika mashindano yote unayoshiriki, unatakiwa kufahamu kuwa wachezaji wanapaswa kubadilishwa.
“Ndicho kinachoweza kutokea, kwamba mchezaji muhimu na nyota kikosini anaweza kukalia benchi kutii mahitaji ya mechi husika.”
Mancini alipigwa butwaa baada ya kikosi chake kupoteza uongozi wa 2-1 hadi dakika ya 87 na hatimaye kufungwa mabao 3-2 Jumanne kwenye dimba la Santiago Bernabeu – walipocheza na wenyeji wao Real Madrid.
Mshambuliaji Mario Balotelli aliwekwa benchi katika mechi hiyo na kuzua utata na sintofahamu kuhusu majaaliwa yake, huku akiwa na uwezekano pia wa kubaki benchi tena kesho wanapoumana na Arsenal katika mechi ya Ligi Kuu.
Mancini alikizungumzia kikosi chake cha kwanza dhidi ya Madrid: “Nilifanya maamuzi bora kwa faida ya timu. Ulikuwa ni uteuzi wa kimbinu zaidi kwa sababu nilitaka kubaki na washambuliaji waili kwenye benchi na watatu wangekuwa wengi zaidi.”
Kocha huyo akajitetea kuwa Balotelli hakufanya vema vya kutosha, wakati akisafiri na timu kwenda Hispania. 
Mancini akaongeza: “Mario alikuwa amechukizwa, lakini nadhani ni jambo la kawaida. Hakuna mchezaji ambaye atafurahi kuachwa bila kucheza kwwenye Uwanja wa Bernabeu.”
Balotelli alianzishwa kwenye kikosi cha kwanza cha City kilichoumana na Stoke wiki iliyopita, lakinia akaonesha kiwango kibovu katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 na kumkera Mancini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...