Mabingwa wa mashindano ya Balimi Ngoma Ngazi ya Mkoa,Mkoa wa Mara,Kikundi cha
Egumba wakicheza wakati wa fainali za Ngoma za Asili zilizofanyika katika Bwalo
la Magereza Musoma mwishoni mwa wiki.Mashindano hayo
yanadhaminiwa na TBL kupitia Bia ya
Balimi Extra Lager kwa mikoa ya kanda ya ziwa tu.
Na Mwandishi Wetu.Mara.
KUNDI LA NGOMA LA EGUMBA MABINGWA
BALINGOMA MKOA WA MARA.
KUNGI la Ngoma la Egumba
wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Ngoma za Asili ngazi ya Mkoa
kwa kanda ya Ziwa Mkoa wa Mara yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania(TBL)
kupitia Bia ya Balimi Extra Lager Kanda ya Ziwa.
Kundi la Ngoma la Egumba
kwa ubingwa huo lilijinyakulia kitita cha fedha taslimu shilingi 600,000/=
pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Mara kwenye fainali za mashindano ya
Kanda yatakayojumuisha Mikoa mitano ya Kanda ya Ziwa ambayo ni
Tabora,Shinyanga,Kagera,Mwanza na Mara,mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika
mwishoni mwa wiki hii jijini Mwanza.
Katika kinyang'anyilo
hicho ambacho kilikuwa na ushindani mkubwa,kundi hilo limeibuka mshindi kwa
alama 66.5 likifuatiwa na kundi la Gari kubwa ambalo imepata alama 64 na
kuondoka na zawadi ya shilingi laki 5 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na
Kiwajaki na kujipatia shilingi laki 300 kwa kupata alama 62,
Katika mpambano huo
ambao umevishirikisha vikundi 9 na kuhuduriwa na idadi kubwa wa mashabiki wa
burudani za ngoma za asili wakiongozwa na Mkuu wa Gereza Musoma
Edson Yalimo , washiriki wote kuanzia nafasi ya 5 mpaka ya 10 wamejinyakulia
zawadi ya fedha tasilimu shilingi laki moja na nusu ambapo mkuu huyo wa Gereza
ameipongeza kampuni hiyo kwa kudhamini mashindano hayo ya aina yake hapa
nchini.
Mkuu Huyo wa Gereza la
Musoma Rpo Edson Yalimo, amesema kuwa kwa kutumia mashindano kama hayo jamii
imekuwa ikiburudika na kutukumbusha tamaduni zetu ambazo mara nyingi
zimekuwa zikisahaulika kwa wengi na kuiomba kampuni ya TBL kuendelea kudhamini
mashindano hayo na kuwataka kutosita kushilikiana na serikali katika masuala
mbalimbali ya kijamii kwa kuwa kwa kufanya hivyo wamekuwa wakisaidia baadhi ya
majukumu ya serikali.
Naye Meneja masoko wa
Kampuni ya bia Tanzani (TBL) kanda ya ziwa Endrew Mbwambo amesema kuwa
kampuni yake imekuwa ikishiriki katika kudhamini shughuli mbalimbali za
kijamii ikiwemo michezo na burudani ikiwa ni shukrani zao kwa jamii kwa kutumia
bidhaa zao ambapo ameiomba jamii ili kampuni hiyo iweze kuendelea kudhamini
shughuli hizo wawaunge mkono kwa kutumia bidhaa zao.
Vikundi vingine
ambavyo vimeshiriki katika fainali hizo ni pamoja na Nyakitali, Victoria
,Maisha Bora,Musoma One,Mshikamano naKiwasabu ambapo Tarehe 20 mwezi huu
itafanyika fainali hizo katika mkoa wa Mwanza,
No comments:
Post a Comment