Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa Al
Madrassatul Munauwaratul Islamiya iliyopo Msasani Bonde la Mpunga
Ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kukabidhi
Spika mbili, Vipaza sauti viwili (Microphones) pamoja na Amplifaya
ambavyo vitatumika kuendeshea shughuli mbalimbali za kueneza mafunzo ya
dini kwa jamii na watoto wanaosoma chuoni hapo. Vifaa hivyo vimetolewa
na mdau mpenda maendeleo kupitia kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala
Jerry Silaa.
Pichani
juu na chini ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pamoja
na Bw. Abdulmalik Ibrahim (kulia) aliyemwakilishi mdau aliyetoa vifaa
hivyo (jina kapuni) wakikabidhi Spika tatu, vipaza sauti viwili na Mixer
kwa Katibu wa Madrasa hiyo Bw. Salim Amri (wa pili kushoto)
aliyeambatana na Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah (katikati). Kushoto ni
mmoja wa walimu wa madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani
Bonde la Mpunga Ustaadh Mohamed Kassim.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akikagua moja vifaa hivyo alivyokabidhi leo ofisini kwake .
Ustaadh
Nurdin Nassor Abdallah wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya ya
Msasani Bonde la Mpunga akitoa shukrani kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa
pamoja na mdau alijitolea baada ya kupokea vifaa hivyo ambavyo amesema
vitawasaidia katika kazi zao za kueneza neno la Mungu hasa kipindi hichi
cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo kuhubiri Amani nchini.
Uongozi
wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la
Mpunga wakiomba dua za baraka kwa msaada waliopokea leo ofisini kwa
Mstahiki Meya Jerry Silaa.
No comments:
Post a Comment