Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 10, 2013

TASWA QUEENS YAIFUNGA 38-9 WALIMU QUEENS


Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Netiboli ya waandishi wa habari nchini ‘Taswa Queens’ juzi iliendeleza makali yake ya kutofungwa baada ya kuwagaragaza walimu wa shule ya Mkuranga katika ziara ya kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Jahazi la magori la Taswa Queen lilinogeshwa na Mshambuliaji hatari Sharifa Mustapha wa Majira akisaidiana na Kiungo mchezeshaji ambaye pia ni nahodha wao timu hiyo Oliver Alobogast wa Mwananchi na kuukaribisha vyema Mwenzi huo  kwa kuwafunga walimu hao magoli 38-9.

Kikosi hicho kinachonolewa na Zainabu Ramadhani na Amina Musa kilianza kilijikuta kikishangiliwa kwa hali ya juu na Mashabiki wa timu ya Walimu kutokana na mpira safi waliouonyesha dimbani na kipindi cha kwanza kuongoza kwa magoli 20-2.

Ushindi huo wa awali uliwafanya wachezaji hao kuongeza juhudi ambapo mpaka mwamuzi anamaliza mchezo huo Taswa Queens iliibuka kidedea kwa magoli 38-9.

Kikosi cha Taswa Queen kilichofanikisha ushindi huo ni pamoja na Sharifa Mustapha (GA), Zainabu Ramadhani (GS), Farida Husseni(GD),Charity James(GK), Zuhura Abdunoor(WD), Clezencia Tryphone(WA) na Olver Alobogast(C) huku Elizabeth John na Zaituni Kibwana wakianzia bechi.

Mbali ya Taswa Queens kuibuka na ushindi huo mfululizo kwa upande wa Taswa FC, wao bundi anazidi kutanda katika kikosi chake mara baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa timu ya Wanaume wa Walimu hao licha ya mpambano kutomalizika mara baada ya kutokea kwa sintofahamu baada ya mchezaji wa Taswa Zahoro Mlanzi kutoka Jamboleo akizichapa kavukavu na mmoja wa wachezaji wa timu pinzani kwa madai ya kumchezea rafu za mara kwa mara na kusababisha mwamuzi kumaliza mpambano zikiwa zimesalia kama dakika 10 kipindi cha pili.

Mwenyekiti wa timu hiyo Majuto Omari alisema, vijana wake walistaili kushinda mpambano huo na kudai kuwa kuvunjika kwa pambano ndo sababu ya matokeo hayo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...