Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 25, 2013

Washindi wa Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ wakabidhiwa Bajaji zao


 Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi wa kwanza wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’, Bw. Mohamed Ramadhani Mnjori (39) muuz nguo za mitumba, mkazi wa Ilala – Dar es Salaam kwenye halfla ya makabidhiano iliyofanyika eneo la Soko Kuu la Kariakoo, Dar es Salaam.
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (kushoto) akimpa mkono wa pongezi mshindi wa kwanza wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’ ibuka na Bajaji Bw. Mohamed Ramadhani Mnjori (39) alipopanda kukagua Bajaji yake. Bajaji hiyo ina thamani ya Tsh 6,700,000.
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi wa pili wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’, Bw. Riziki Lucas Kisemo (36) mfanyakazi wa viwandani, mkazi wa Makabe, Dar es Salaam. Tigo tayari imelipia leseni ya barabani (Road license) na bima kwa ajili ya Bajaji hizo. Anachotakiwa mteja sasa, ni kuanza biashara yake bila shida mara moja. 
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga akimtambulisha mshindi wa tatu wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’ Bw. Adam Saidi Kalulu (36) mkulima, mkazi wa Kiluvya kabla ya kumkambidhi Bajaji yake mpya mbele ya wanahabari na wananchi waliojitokeza eneo la Soko Kuu la Kariakoo kushudia makabidhiano hayo.
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (mwenye kofia ya Tigo) katika picha ya pamoja na washindi watatu wa kwanza ya promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’ ibuka na Bajaji wakati wa sherehe ya makabidhiano iliyofanyika leo eneo la Soko Kuu, Kariakoo. Mteja wa Tigo anao uwezo wa kujishindia Bajaji moja kila siku kwa muda wa siku 60 kwa kuongeza vocha ya Tsh 1,000 tu kwa siku.
Mshindi wa pili wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’, Bw. Riziki Lucas Kisemo (36) mfanyakazi wa viwandani, mkazi wa Makabe, Dar es Salaam akitoa ushuhuda mbele ya vyombo vya habari jinsi hapo zamani alipokuwa akihangaika na kazi ‘ngumu ngumu’ ambazo zilikuwa hazimpi kipato cha kutosha cha kuendeshea maisha yake. Mshindi huyo ametoa shukurani nyingi sana kwa Tigo na ametoa rai kwa watanzania wengine waweze kushiriki. “Hakika Tigo imebadilisha maisha yangu,” Riziki alisema. Pembeni yake ni Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga,

Bajaji 3 kati ya Bajaji 60 zilizoshindwa na washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’ zikipaki eneo la Soko Kuu, Kariakoo kabla ya kukabidhiwa kwa washindi mapema leo. Zimebakia Bajaji 57 zakushindaniwa, droo inayofuata itachezwa siku ya Jumatatu 29 Julai, 2013 kwa ajili ya kuwapata washindi 7 wa wiki hii. Wateja wanaweza kuendelea kushiriki kwa kuongeza salio mara nyingi wawezavyo ili kujiongezea nafasi zaidi ya kujishindia Bajaji na kumiliki biashara zao wenyewe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...