Omari Kimweri |
BONDIA Mtanzania Omari
Kimweri 'Lion
Boy' anaefanya shughuli zake nchini Australia anatarajia kupanda
ulingoni mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya kuchezo mpambano wake
mwingine baada ya kuwatwanga mabondia kadhaa nchini humo bondia huyo
anaechezea uzito wa light flyweight
Amesema kuwa ataendeleza wimbi la ushindi kwa kutoa vipigo kama alivyotoa kwa bondia Yodpichai Sithsaithong pamoja na Lookrak Kiatmungmee ambazo ndio mechi zake za mwisho kucheza kabla ya hii inayomkabili punde
Aliongeza kwa kusema kuwa unajua mimi ni
Bingwa hivyo sito kubali kupoteza mpambano huo utakaofanyika katika
ukumbi wa The Melbourne Pavilion nchini Australia mpambano huo
utakaosimamiwa na kamisheni ya nchi hiyo umekuwa gumzo kila kona kwa
kuwa bondia Mtanzania Kimweri amejizolea umaarufu mkubwa nchini humo
Bondia huyo aliyeanza kujishulisha na mchezo wa ngumi za kulipwa nchini Australia mwaka
2007 Mpaka sasa akiendelea na shughuli zake hizo amesema lengo lake kubwa ni kuchukuwa mikanda inayotambulika kimataifa ingwa yeye kwa sasa ni bingwa wa WBO ambapo aliupata kwa kumtwanga bondia Panmongkol Ekarin wa Thailand bondia huyo amewaomba watanzania kumuombea duwa kwani ana kibarua kizito cha kuitanganza nchi yake kimataifa bondia huyo mwenye uraia wa nchi mbili Tanzania na Austalia amesema ana mpango wa kuja Tanzania na kuzamini mchezo uho kama mfadhili endapo marengo yake yatatimia alisema 'mimi nataka nije kupigana Tanzania nikiwa mchezaji na promota vile vile hivyo nafanya mpango huo mambo yakiwa mazuri nitakuja bongo ili nifanye uwekezaji katika Boxing '
Bondia huyo mpaka sasa amekwisha cheza
mapambano 15 akishinda 12 na kupoteza mapambano matatu bondia huyo
anayefananishwa na Simba muwindaji amekuwa tishio kwa mabondia wenye
uzito wake kwa niaba ya watanzania wote tunaungana kumsapoti bondia
Omari Kimweri anayefanya kazi zake nchini Austalia aweze kushinda
mpambano waku huo Mungu Ibariki Africa,Mungu Ibariki Tanzania, Mungu
Mbariki Bondia Omari Kimweri, AMIN
Bondia Mtanzania Omari Kimweri akinyooshwa mkono juu kuashiria ushindi wake |
No comments:
Post a Comment