Promota wa mpambano wa masumbwi Side Mkigoma (katikati) akiwainua mikono juu mabondia Juma Fundi (kushoto) na Nassibu Ramadhani.
Na Mwandishi Wetu
BONDIA
Nassibu Ramadhani amejigamba kuwa atamchakaza mpinzani wake Juma Fundi
wakati wa mpambano wao utakaopigwa siku ya Idi pili katika ukumbi wa friends corner Manzese
Aliongeza kwa kusema unajua mimi
anaeniumiza kichwa kwa sasa ni Fransic Miyeyusho pekee kwa Tanzania hii
kwa kuwa nilicheza nae na nikashindwa kummudu ata hivyo ipo siku
nitaomba mpambano mwingine wa marudiano nae hivyo nimemuweka kiporo
Bondia huyo aliendelea kujinasibu kwa
kusema kwa sasa mimi ni nambari One hivyo fundi ategemee kipigo cha mbwa
mwizi kwa ni ato furukuta
Naomba mashabiki wangu wa ngumi
mjitokeze kuja kunishangilia ata kama wewe sio shabiki wango njoo uone
ngumi nitakazokuwa nikicheza na utamini kuwa mimi ni kiboko yao
Ramadhani ambaye ucheza kwa kasi kubwa
sana awapo ulingoni amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki na kumpachika
jina la Mann Paquaio wa Philipins kwa kuwa wote wanatanguliza mguu wa
kulia mbele
Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD
mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zatakazokuwa zikisabazwa
na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila
'Super D'
pia siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi wakisindikiza mpambano huo
No comments:
Post a Comment