
Na Elizabeth John
KINDA
 anayetamba katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini, Abdulaziz 
Chende ‘Dogo Janja’ anatarajiwa kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa 
jina la ‘Serebuka’ hivi karibuni.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Dogo Janja alisema ngoma hiyo ameshaikamilisha na anatarajia kuanza kuisambaza katika vituo mbalimbali wiki ijayo.
Alisema
 yuko katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho ambacho anaamini
 kitakonga nyoyo za mashabiki wa muziki huo ndani na nje ya nchi 
kutokana na ubora wa mashairi yaliyopo ndani yake.
“Namshukuru
 Mungu kazi zangu huwa zinapokewa vizuri na mashabiki wangu, kitu 
ambacho kinanipa moyo wa kuendelea kufanya vizuri katika ‘game’, hivyo 
nawaomba mashabiki wa kazi zangu waendelee kusubiri vitu vizuri kutoka 
kwangu,” alisema Dogo Janja.
Mbali na kibao hicho, Dogo Janja kwasasa anatamba na kibao chake cha ‘Maisha ya Skonga’ ambacho ameshirikiana vema na mwaamuziki kutoka kundi la Watanashati, PNC na kwamba ameamua kushirikiana naye kutokana na uwezo wake katika tasnia ya muziki, ikiwa ni pamoja na historia yake nzuri ya kuutangaza muziki wa Bongo.
No comments:
Post a Comment