Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 28, 2013

LINDI SOCCER ACADEMY WAVULIWA UBINGWA COPA COCA COLA MANISPAA YA LINDI


Kikosi cha Lindi Soccer Academy (LSA) kilichoshiriki michuano ya Copa Coca Cola 2013. Wa kwanza kushoto waliosimama, ni Ofisa Habari wa LSA, Salum Mkandemba, ambaye pia ni Mhariri wa Habari Mseto Blog. Aliyesimama kulia ni Mkurugenzi wa LSA, Hafidh Karongo na wa kwanza kulia aliyekaa ni Meneja wa Double M Hotel ya mjini Lindi ambako LSA huweka kambi za mazoezi.

LINDI, Tanzania

Licha ya kuvuliwa ubinwa, LSA imeendelea kutawala kikosi cha Copa Coca Cola Kombaini Manispaa ya Lindi, baada ya kutoa jumla ya vijana 16 katika kombaini hiyo inayotarajiwa kuingia kambini kesho Jumatatu kujindaa na michuano ya Copa Coca Cola mkoa wa Lindi itakayofanyika baada ya mfungo wa Ramadhani

TIMU ya Lindi Soccer Academy (LSA), jana imevuliwa ubingwa wa michuano ya Fifa Copa Coca Cola Manispaa ya Lindi, baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Cariacops, katika fainali ya michuano hiyo iliyokuwa ikifanyika kwenye Uwanja wa Ilulu, mjini Lindi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa LSA, Hafidh Karongo, Cariacops katika mechi hiyo iliibuka kidedea ikibebwa na mabao ya mapema ya wakali wake George Muta aliyefunga katika dakika ya nane na James Masheyo dakika ya 30.

Licha ya mabadiliko kadhaa katika jitihada za kujinasua, LSA ilimaliza pambano hilo kwa kipigo hicho, kilichohitimisha kipindi chao cha ubingwa waliotwaa mwaka jana, ingawa imeendelea kutawala kikosi cha Copa Coca Cola Kombaini, Manispaa ya Lindi.

Karongo aliiambia Tanzania Daima kwa simu kuwa, LSA imetoa jumla ya vijana 16 katika Kombaini ya Manispaa ya Lindi, inayotarajiwa kuingia kambini leo kujindaa na michuano ya Copa Coca Cola mkoa wa Lindi itakayofanyika baada ya Ramadhani.

Aliwataja chipukizi walioteuliwa kuunda Kombaini hiyo kuwa ni; Harid Selemani, Shaffih Maulid, Ramadhani Amri, Hassan Mkomba, Hassani Alubuni, Joseph Keneth, Mohammed Omari, Hamis Mahmoud, Midraji Haji na Ramadhani Bakari.


Wachezaji wengine wa LSA ni pamoja na; Rajabu Msela, Abdul Shein, Hamdani Sarahani, Hassan Pendeka, Banzalam Hamisi na Yassin Abdallah ‘Iniesta.’ Timu nane zilishiriki Copa Coca Cola Manispaa ya Lindi na kugawanywa katika makundi mawili.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...