Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema, akimkabidhi zawadi yenye nembo ya Jeshi Polisi Tanzania, Naibu Kamishina wa UNAMID Dkt. Syed Kaleem Imam, kutoka nchini Sudan, jimbo la Darfur, alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam, akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku sita hapa nchini.
Naibu
Kamishina wa UNAMID Dkt. Syed Kaleem Imam, kutoka nchini Sudan, jimbo
la Darfur (wapili kutoka kulia), akitoa mada katika kikao cha
kubadilishana uzoefu kilichowashirikisha makamishina na maofisa
waandamizi wa Jeshi la Polisi Nchini. Kutoka kulia ni Kamishina wa
utawala na fedha wa jeshi la polisi, CP Clodwig Mtweve, Kamishina wa
Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Paul Chagonja, Mkuu wa
tathmini na ufuatiliaji Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) Omar Rashid
pamoja na Mkuu wa Utawala na rasilimali wa jeshi la Polisi (DCP)Thobias
Andengenye.( Picha na Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi Dar es salaam.)
No comments:
Post a Comment