Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 21, 2013

MEYA WA JIJI LA ILALA MH. JERRY SILAA AFANYA ZIARA KATIKA MASOKO YA ILALA NA BUGURUNI KUKAGUA BEI ZA BIDHAA KIPINDI HIKI CHA MFUNGO WA RAMADHAN

.

IMG_9312  
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa ( wa nne kulia)akipata maelezo kutoka mmoja wa wafanyabiashara wa mihogo Ilala alipofanya ziara rasmi katika masoko ya Buguruni na Ilala kuangalia utofauti bei za bidhaa kabla na kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mstahiki Meya aliwaasa wafanyabiashara kutokupandisha bei ya bidhaa mbalimbali wakati mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuwawezesha Waislamu wa mkoa wa Dar kuwa na mfungo mwema na wao pia kupata Thawabu kwa Mwenyezi Mungu kwani watawezesha hata wale wenye kipato cha chini kumudu bei bidhaa zinazotengeneza futari. Mh. Silaa amewatembelea wafanyabiashara katika masoko kuangalia uwiano wa bei katika masoko hayo.
IMG_9295
IMG_9315
IMG_9286
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiendelea na ziara yake kwenye masoko katika halmashauri yake ya Ilala akiwa ameambatana maafisa wa mbalimbali wa Manispaa ya Ilala.
-- Zainul A. Mzige, Operation Manager, MO BLOG, www.mohammeddewji.com/blog +255714940992.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...