Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 18, 2013

Wanahabari watembelea Mradi wa Uranium uliopo chini ya Kampuni ya Manrta Tanzania,Namtumbo Mkoani Ruvuma leo


 Afisa wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania inayoshughulika na Mradi wa Uchimbaji Madini aina ya Uranium,uliopo kwenye Kijiji Mkuju,Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma,Fredrick Kriel akitoa mada ya maswala ya Usalama Mgodini wakati wa Semina fupi kwa Baadhi ya Wanahabari waliofanikiwa kutembelea Mradi huo uliopo pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seluu na kufahamu mambo mbali mbali juu ya Madini hayo ya Uraniuam.
Afisa wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Fredrick Kriel akionyesha moja ya mambo muhimu na yanayotakiwa kuzingatiwa kwa mtu yeyote awapo Mgodini.
Meneja Mkuu wa Maswala ya Usalama, Afya, Mazingira na Ubora wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Cornelis Van Den Berg akifafanua jambo kuhusu mradi huo wa Madini ya aina ya Uranium wakati wa semina fupi na baadhi ya Wanahabari walioweza kutembelea Mgodi huo leo,na kuweza kujionea na kufahamu mambo mbali mbali juu ya Mgodi huo.
Mkuu wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija Palangyo akielezea namna Kampuni yake inavyoweza kutoa kipaumbele katika kusaidia jamii inayouzunguka mradi huko.
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wahusika wa Mradi huo.Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda ambaye ameambatana na wanahabari hao,na wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija Palangyo.
Sehemu ya Mandhali ya Mahema ya maofisi ya Kampuni hiyo wakati huu wa Utafiti wa Madini ya aina ya Uranium.
Wanahabari hao wakiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wasimamizi wa Mradi huo.
Afisa wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Fredrick Kriel akitoa maelezo ya namna mambo yanavyokuwa pindi wawapo kazini.Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda na kushoto ni Mwanalibeneke Othman Michuzi wakisikiliza kwa umakini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...