HALI
ya mambo imeanza kuwa mbaya baada ya kuenea kwa habari kuwa baadhi ya
wananchi wa mjini Mtwara waliivamia gari lililobeba mabomba ya gesi
kutoka mjini humo.
Gari
hilo lilikuwa limebaba mabomba hayo kutoka Mjini Mtwara kuelekea jijini
Dar es Salaamlimeshambuliwa na mawe na kupelekea dereva wa lori hilo
kujeruhiwa vibaya na kuibua taharuki.
Lori
hilo lilianza kushambuliwa mara baada ya kuingia katika Manispaa ya
Mikinda Mtwara Mjini sababu ya kushambulia gari hilo ni katika kile
kinacho dhihirisha kuwa wanamtwara bado hawajakubaliana na hoja ya Serikali ya kutaka kusafirisha gesi hiyo kwa ajili ya manufaa ya nchi.
Lori hilo kwa sasa lipo kituo kikubwa cha polisi Mtwara, ikiwa
ni wiki moja tu imepita tokea watu kadhaa kukamatwa na jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kile kinachodaiwa kusambaza waraka wa kuhujumu miundombinuu yote ya gesi mara tu serikali itakapo anza utekelezaji wake wa ujenzi wa bomba hilo kupeleka jijini Dar es Salaam kama ilivyokubaliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment