Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Magu, Aileen
Geofrey akimwonyesha kwa kuandika ubaoni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Mahusiano na Uratibu Stephen Wasira kwamba anajua kusoma na kuandika, baada ya
Waziri Wasira kumuuliza kama anajua mambo hayo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Magu, Jacqueline Liana Waziri Wasira alikuwa wilayani
Magu, mkoani Mwanza juzi (24.7.2013) kwa ziara ya siku moja kukagua miradi ya
maendeleo.
Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wajasiriamali
cha Tujikomboe wilayani Magu, Maria Mwita akimweleza Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Mahusiano na Uratibu Stephen Wasira,shughuli mbalimbali zinazofanywa na
kikundi hicho, Waziri Wasira alikuwa katika ziara ya siku moja wilayani Magu,
mkoani Mwanza
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na
Uratibu, Stephen Wasira,akimpongeza baada ya kumkabidhi hati ya kukamilisha
mradi wa jamii Mwenyekiti wa Mtaa wa Ibidanja Ponsian Garimo,baada ya kukagua
madarasa matano ya Shule ya Msingi Magu ambayo yalijengwa na TASAF kwa
kushirikiana na wananchi. Waziri Wasira alikuwa wilayani Magu, mkoani Mwanza
juzi (24.7.2013) kwa ziara ya siku moja kukagua miradi ya maendeleo
WACHEZAJI wa kikundi cha utamaduni cha
Mwanalyaku Cultural Troupe cha wilayani Magu, mkoani Mwanza, wakitoa burudani
wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen
Wasira alipotembelea juzi (24.7.2013) kijiji cha Kitongosima kilichopo katika
wilaya ya Magu, mkoani Mwanza, kukagua shughuli za maendeleo.
No comments:
Post a Comment