Mgeni
Rasmi katika hafla ya utoaji wa msaada , Rais Mstaafu Alhaji Ali
Hassan Mwinyi (kulia) akitoa hotuba katika hafla hiyo leo jijinji Dar es
salaam (kushoto) ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaaam, Alhadi Mussa
Salum. Katika hafla hiyo, UAE imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa jumla
ya watoto 5000 wa nchini Tanzania.
Baadhi ya watoto waliohudhuria katika hafla leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ,Bibi Kijakazi
Mtengwa akisoma risala katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Rais
Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akimpongeza mtoto baada ya kumpatia
msaada wa nguo na viatu uliotolewa na Mf uko wa kusaidia watoto wenye
mahitaji maalumu kutoka Umoja wa nchi za Kiarabu (UAE )Charity.leo
jijini Dare es salaam.(pichani kushoto) ni Mwenyekiti wa Mamlaka ya
masuala ya Kiislam na Mjumbe wa Bodi ya Red Cresent Dkt. Hamdan Al-
Mazroei na (kulia)Mwakilishi wa Balozi wa UAE nchini Tanzania Mohamed
Alzaabi.
Rais
Msataafu Alhaj Hassan Mwinyi (mwenyekoti jeusi) , Mwenyekiti wa The
General Authority for Islamic Affairs And Endowments na Mjumbe wa Bodi
ya Red Crescent kutoka UAE Dkt. Hamdan Al Mazroei (kushoto) pamoja na
Mwakilishi wa Balozi wa UAE nchini Bw, Mohamed Alzaabi (kulia)
wakiwapongeza baadhi ya watoto baada ya kuwakabidhi msaada wa nguo na
viatu leo jijini . Jumla ya watoto 5000 watapata msaada huo ikiwemo
mikoa ya DSm 1500.Arusha 1500, Tanga 1000 na Zanzibar 1500.
Baadhi ya watoto wakiingia katika jengo la Ubalozi wa UAE nchini Tanzania kuhudhuria hafla hiyo.
Mwenyekiti
wa Mamlaka ya Masuala ya Kiislam na Mjumbe wa Bodi ya Red Crescent
kutoka UAE akiongea leo katika hafla ya kuwakabidhi msaada kwa watoto
wenye mahitaji maalumu nchini Tanzania, Jumla ya watoto 5000
wamebahatika kupata msaada huo wa nguo na viatu, Mfuko wa kusaidia
watoto wenye mahitaji maalumu ulianzishwa tarehe 19 mei ,2007 na Makamu
wa Rais wa UAE Shaikh, Muhammed bin Rashid Al Maktoum, ukiwa na thamani
ya dola za kimarekani 10 bilioni.
Mwenyekiti
wa Mamlaka ya masuala ya Kiislam na mjumbe wa Bodi ya Red Crescent
Dkt. Hamdan Al- Mazroei (kulia) akiwapa msaada wa nguo na viatu
wanafunzi wa Alkhairat Islamic Center ya Mabagala jijini Dar es Salaam
,leo katika hafla hiyo ambapo mgeni Rasmi alikuwaRais Msataafu Mzee Ali
Hassan Mwinyi (hayupo pichani) PICHA ZOTE NA MWANAKOMBO JUMAA-MAELEZO.
No comments:
Post a Comment