Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, July 23, 2013

SEMINA KUHUSU USALAMA WA MATUMIZI YA KOMPYUTA (CYBER DEFENCE) KUFANYIKA MOROGORO


Rais wa taasisi ya isiyo ya kiserikali ya ISACA tawi la Tanzania, Boniface Kanemba akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kuhusu semina inayohusu usalama wa matumizi ya mitandao ya kompyuta ‘Cyber Defence East Africa 2013 itakayofanyika Julai 28 mjini Morogoro.  Kulia ni, Ofisa Mtendaji  wa Norway Registers Development (NRD), kwa nchi za Afrika Mashariki, Sebastian Marondo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
DAR ES SALAAM, Tanzania

ISACA Tanzania chapter pamoja na NRD East Africa wameandaa semina inayohusu usalama wa matumizi ya kompyuta na  mitandao yake katika nyanja zote. Semina hii ijulikanayo kama Cyber Defense East Africa 2013 itakayofanyika Tar 28 -30 mwezi wa nane pale nashera hoteli Morogoro. Mafunzo haya ambayo yatafunguliwa na naibu waziri wa mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh January Makamba yamelenga kwa kina kutoa mafunzo kwa waatalamu wa TECHNOHAMA haswa wale wanaohusika na usalama wa mitandao hiyo. 

Mafunzo haya ambayo yatawahusisha wataalumu wa makampuni ya usalama  wa mitandao kutoka pande  mbali mbali za dunia yakiwemo makampuni kutoka nchi za ulaya, America na Africa Kusini, FireEye, Fortinet, Lumension, IBM Q1Labs, Qualys, AccessData na Balabit wataongea kwa kina wanachokifanya katika ulinzi na usalama wa mitandao na teknolojia wanazozitengeneza za kudhibiti uhalifu wa mitandao

Vile vile, wataalamu hao wataonyesha kwa vitendo mambo mbali mbali yanayofanyika wakati wa kufanya  wizi wa mitandao, na  washiriki wa semina hii watashiriki kwa vitendo hivyo ambayo vimelenga kutoa ufahamu zaidi juu ya kile kinachotokea kwenye mtandao  haswa kwa matumizi mabaya kama wizi. Kila mshiriki atajionea kwa macho yake jinsi wizi wa mtandao unavyoandaliwa na kufanyika katika maeneo mbali mbali yakiwemo katika mabeki, serikali, makampuni ya simu na mengineyo na hivyo kuongeza ufahamu wa jinsi ya kudhibiti uhalifu.

Mafunzo haya ni kwa ajili ya wadau mbalimbali kutoka secta zote za uma na binafsi na pia kutoka nchi zote tano za Afrika Mashariki, yaani Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burudi. 

Hii ni kutokana na nchi hizi kuwa na changamoto sawa la ongezeko la wizi wa mitandao na matumizi mabaya ya mitandao  katika miaka ya hivi karibuni. Mfano, tafiti iliyofanywa na kampuni ya Deloitte mwaka 2012 inaonyesha kuwa mabeki ya kibiashara kwenye nchi za Africa Mashariki yanapoteza takribani zaidi ya Tsh Bil 80 kutokana na wizi wa mitandao kwa mwaka kiasi ambacho bado kinasadikiwa kuwa kinaweza kuwa ni zaidi ya hapo ikizikatia kuwa matukio mengi huwa haya ripotiwi hivyo kutokuwa na idada kamili ya fedha zote.

Hali kadhalika matumizi ya M-pesa nayo yameongezeka kwa kasi na hivyo kuongeza matukio ya wizi unaohusiana na miamala yake. 

Mbali na wizi wa fedha, makampuni mengi binafsi, umma pamoja na serikali yanapoteza taarifa nyingi sana zikiwemo zile binafsi na nyaraka muhimu za matumizi ya ofisini bila kujua. Taarifa hizo ambazo huchukuliwa kwa kutumia teknolojia ya wizi wa mitandao huishia mikononi mwa wahalifu ambao wanazipembua na kujua siri mbali mbali za makampuni, zikiwemo taarifa za fedha, mipango mikakati kimasoko, utawala na kadhalika.

Ndg waandishi wa habari, tumechukua jukumu hii tukijua kabisa serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu kwa kila mtanzania, ni lazima makampuni na mashirika binafsi tuungane kwa pamoja kuilinda na kuijenga nchi yetu huu ukiwa ni mpango unaoenda sambamba na malengo ya millennia haswa lengo namba 8 “Developing a global partnership for development” lengo ninalosisitiza matumizi zaidi ya mitandao na kuhimiza serikali kushirikiana na secta binafsi kuendeleza  mpango wa maendeleo.

Tunaomba kutumia fursa hii kuishukuru serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano wanatupatia kila mara.

 Pia tunamshukuru Mshimiwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa kutoa muda wake kufungua Mafunzo haya.

Pia tutumie fursa hii kuwahamasisha wadau wote wa TECHNOHAMA kutoka serikali, kwenye Mabenki,Mashirika ya umma na yale ya binafisi na hata mtu mmoja mmoja kujitoa kwa kina kushiriki fursa hii ya mafunzo ya kimataaifa ya usalama wa mitandao.
Nafasi ziko wazi, unaweza kujiandikisha kwenye mitandao yetu au kwa kupiga simu kama inavyoonekana hapa chini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...