Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Angetile Osiah
akikabidhi kombe la ubingwa kwa timu ya Mbaspo kutoka Mbeya baada
ya kufanikiwa kushindwa kwa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya
wahasimu wao Mbeya City katika faili ya kombe la Muungano Mufindi 2013
na kunyakua kombe na pesa kiasi cha Tsh milioni 3
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa
Mbeya kushoto akiwa na mmoja kati ya wachezaji wa timu ya Mbaspo
wakionyesha kombe la ubingwa leo katika uwanja wa shule ya Msingi
Wambi mjini Mafinga
Mabingwa wa mashindano ya kombe la
Muungano Mufindi mwaka 2013 timu ya Mbaspo ya Mbeya katika picha ya
pamoja na mashabiki wageni rasmi na wadhamini jioni ya leo katika
uwanja wa Wambi mjini Mafinga
Timu ya Mbaspo kutoka mkoani Mbeya
leo imeibuka bingwa wa mashindano ya kombe la Muungano 2013 baada
ya kuigagadua kwa jumla ya mikwaju ya paneta 5-4 timu ya Mbeya
City katika mchezo wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Shule
ya Msingi Wambi mjini Mafinga mchezo ulioshuhudiwa na mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Angetile Osiah.
Katika mchezo huo
timu zote mbili ziliweza kuonyesha soka kali lililofanya mashabiki
kujigawa katika kuzishangilia timu hizo ambazo zote mbili zilikuawa
katika uwanja wa ugenini.
Mbali ya timu ya
Mbeya City kujipatia mashabiki wengi kipindi cha kwanza wa
kuishangilia ila hali iligeuka na mashabiki robo tatu ya uwanja
kuamua kuelekeza ushabiki wao kwa timu ya Mbaspo kutokana na viungo
wake nambali 4 na 14 mgongoni kuuteka uwanja huo kwa soka safi.
Hadi timu zote mbili zinakwenda mapumziko kipindi cha kwanza hakuna timu iliyobahatika kuchungulia lango la mwenzake .
Kasi ya mchezo
ilionekana kubadilika kipindi cha pili kwa timu zote kukamiana bila
mafanikio hadi mwamuzi wa mchezo huo alipopuliza filimbi ya mwisho
kuhitimisha mchezo huo bila bingwa kupatikana .
Ili kuwa kazi ngumu
katika upigaji mikwaju ya penati ambapo timu ya Mbeya City ilijikuta
akipoteza nafasi moja na kutoa nafasi kwa timu ya Mbaspo ambao
walijipanga vema na kufanikiwa kuingiza nyavuni mikwaju yote mitano
na hivyo kufanikiwa kuibuka bingwa kwa kuingiza nyavuni mikwaju 5-4
na kufan ikiwa kutangazwa mabingwa katika michuano hiyo.
Katika mashindano hayo
mshindi wa kwanza timu ya Mbaspo imekabidhiwa pesa kiasi cha Tsh
milioni 3 Mendani na kombe ,mshindi wa pili Mbeya City akinyakua
mendani na Tsh milioni 1.5 wakati mwamuzi bora na mchezaji bora kila
mmoja akinyakua Tsh 400,000
Mratibu wa mashindano
hayo Daud Yassin Amewapongeza wadhamini wa mashindano hayo ikiwemo
kampuni ASAS LTd ya Iringa,kampuni ya Mwananchi
Communication,NSSF,Pareto,Ibrahim Khamis, PPF,MUcoba Benk na Chai Bora
kwa kufanikisha mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment