Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, February 4, 2014

DK. SHEIN AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA INDIA, AWEKA SHADA LA MAUA MAKUMBUSHO YA MAHATMA GHANDHI Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Balozi wa Tanzania nchini India John W.H.Kijazi walipofika katika Makumbusho ya Mahatma Ghandhi Mjini New Delhi India na kuweka shada la maua katika makumbusho hayo, akifuatana na ujumbe wake katika ziara ya siku tatu nchini humo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed  Shein akifuatana na ujumbe wake wakielekea katika sehemu maalum iliyotengwa kwa shuhuli ya uwekaji wa maua kwa wageni mbali mbali wanaofika sehemu hiyo ya Makumbusho ya Mahatma Ghandhi mjini New Delhi India.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed  Shein na mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiweka shada la maua katika Makumbusho ya Mahatma Ghandhi Mjini New Delhi, ambayo ni sehemu maalum iliyotayarishwa kwa  wageni mbalimbali wanaofika katika Makumbusho hayo, Rais akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake nchini India. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na ujumbe wake wakiomba dua baada ya wakiweka shada la mauwa  katika   Makumbusho ya Mahatma Ghandhi Mjini New Delhi, akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake nchini India.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed  Shein akiweka saini kitabu cha kumbukumbu ya wageni katika Makumbusho ya Mahatma Gandhi katika Mji wa New Delhi India   baada ya  kuweka shada la mauwa (katikati) ni mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja Balozi wa Tanzania Nchini India John W.H.Kijazi (kulia).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed  Shein akizungumza na mwenyeji wake  MakamU wa Rais wa India Mohammed Hamid Ansari, mara alipowasili  Ofisini kwake Mjini New Delhi,akiwa na ujumbe aliofuatana nao wakiwemo Mwaziri mbali mbali na makatibu. (Picha na Ramadhan Othman, India)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...