Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 3, 2014

TCRA Yawasilisha TSHS. 1.6 Bilioni Malipo ya Kwanza Serekalini kutokana na mtambo wa TTMSWaziri wa Fedha, Saada Mkuya (katikati) na Naibu Katibu Mkuu, Elizabeth Nyambibo (kushoto) wakipokea jana Dar es Salaam, mfano wa hundi ya Sh bilioni 1.6 kutoka  kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma, ikiwa ni gawio kutoka TCRA kutokana na makusanyo ya  kampuni za simu tangu Oktoba mwaka
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  Prof. John Nkoma akitoa Maelezo kwa  Waziri wa Fedha kabla ya kukabidhi hundi ya Mapato ya Mtambo wa Mawasiliano wa TTMS.
 Prof. John Nkoma akitoa Maelezo kwa Waziri wa Fedha kabla ya kukabidhi hundi ya Mapato ya Mtambo wa Mawasiliano wa TTMS.baada ya Prof. Nkoma, ni wakurugenzi wa TCRA alioambatana nao ambao ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Alinanuswe Kabungo, Mkurugenzi wa ICT wa TCRA Dr. Joseph Kilongola na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha Bw. Wilfred Maro

Na Innocent Mungy
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, imetoa malipo ya kwanza ya mtambo wa TTMS (mtambo Maalum wa usimamizi wa Mawasiliano ya Simu) kwa serekali Kufuatia kukamilika Kwa mtambo huo na kuanza kufanya kazi tangu mwezi Oktoba mwaka jana.


TCRA iliwasilisha fedha hizo Hazina, Kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, tukio hilo likishuhudiwa na Waziri wa Fedha Mheshimiwa Saada Mkuya.


Akizungumza katika ghafla ya kukabidhi hundi ya kwanza ya mapato hayo kwa Serekali, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John S. Nkoma alimweleza Mh. Waziri wa fedha kuwa, TCRA imekamilisha kuujenga mtambo huo na umeanza kufanya Kazi tangu mwezi Oktoba mwaka jana 2013. Cheki hiyo ni mapato ya mwezi huo wa Oktoba ambapo kiasi cha shilingi 1,688,299,014.40 zimelipwa kwa serekali kufuatia maelekezo ya Kanuni za TTMC kuwa serekali inapata  28% ya mapato ya simu zinazopigwa kutoka nje ambayo ni cent 7 ya dola kwa dakika.


Mgao wa mapato ya mtambo huo uliojengwa TCRA KWA mfumo wa BOT (Build, Operate and Transfer) umefanikiwa kuongeza pato la serekali baada ya wataalamu wanashiriki ana na TCRA katika mradi huu kufanikiwa kupata cent 25 ya dola KWA dakika toka kwa makampuni ya nje yanayotumika kupiga simu Tanzania, awali Tanzania ikipata cent 8 tu ya dola KWA dakika.


KWA mujibu wa Kanuni hizo, Makampuni ya Simu hupata 52% ya mapato (senti 13 kati ya25) Serekali 28% (senti 7 ya dola katika 25) na Mwekezaji katika mradi huo SGS ya Uswiss hupata asilimia 20%(senti 5 ya dola kati ya 25).


Akizungumza katika ghafla hiyo, Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya aliipongeza TCRA KWA kufanikisha mradi huo na kutoa gawio la kwanza
kwa serekali KWA uaminifu. Aidha alisema mradi huo utakaoongeza mapato ya serekali, uende she vizuri ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo KWA wafanyakazi wanafanya Kazi katika kitengo cha TTMS ili kuwa na weledi zaidi.

Aidha Prof. John Nkoma alimkabidhi Mheshimiwa Waziri pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha cheki ingine ya shilingi 1,625,000,000 (shilingi bilioni moja na milioni Mia Sita) kama sehemu ya maagizo ya Sheria ya Fedha ya Mwaka 2008 inavyoelekeza kuwa Taasisi za Serekali zinazokusanya mapato kutoa asilimia 10% ya mapato ghafi ya makusanyo yake kwa serekali.


Profesa Nkoma akikabidhi cheki hiyo ya pili kwa Viongozi wa Wizara ya Fedha alisema, TCRA
kwa mujibu wa sheria hiyo, umekuwa ikitimiza wajibu wake kwa serekali bila kuchelewa Na KWA mwaka huu wa fedha tayari TCRA ilishatoa tena cheki yenye thamani kama hiyo kwa robo mwaka ya kwanza na imebaki malipo ya robo ya tatu na ya nne KWA mwaka huu wa fedha.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...