Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, February 1, 2014

SKENDO ZA NGONO ZAWAZURIA JAMBO BONGO MOVIE KWA WAKATOLIK



hiyo ya Sister Marry.
KANISA la Romani Katoliki limeishukia tasnia ya filamu Bongo (Bongo Movies) kutokana na matendo maovu yanayofanywa na wasanii katika sinema zao hususan suala zima la kuheshimu imani za watu.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Thadeus Ruwa’ichi.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Thadeus Ruwa’ichi amewaonya wasanii kuwa maigizo yao yasilenge kuchafua umma ama kikundi chochote kwani wanaweza kuleta mgawanyiko katika taifa.
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.

Akizungumzia msimamo wa kanisa kuhusiana na filamu ya Sister Maria ya mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ ambayo kanisa hilo liliipinga kutokana na madai ya kukiuka maadili, Askofu Ruwa’ichi alisema hawakubalini nayo kwani mavazi ya masista yaliyotumiwa na wasanii hao, yalitumika vibaya hivyo hawakubaliani nayo.
Cover la filamu h
Akifafanua zaidi kuhusiana na filamu hiyo, kiongozi huyo wa kiroho alisema alisononeshwa na kazi hiyo ambayo ilikuwa na dosari za kuingilia imani ya kikatoliki kwani mavazi ya kanisa yalitumika kuvaliwa bila staha.
“Ile filamu ilikuwa na lengo la kuhatarisha jamii, kamwe isiendelee kwani ni hatari kwa watu ama mtu binafsi anayechukizwa na tatizo hilo,
“Maigizo yanayofanywa yanaweza kuwa na lengo la kutumbuiza, lakini kutumbuiza kokote kule, hakupaswi kuhatarisha lengo la kulea ama kuvuruga mambo ya watu fulani, kulinda heshima ya watu binafsi ama taasisi, nidhamu inahitajika kwa kila jambo wanalolifanya,” alisema.
Baadhi ya vipande vilivyomo katika filamu hiyo.

Askofu huyo alisema taifa lina mambo mengi na linajivunia kwa amani ya muda mrefu, hivyo waigizaji hao wanapoigiza maigizo ambayo yanagusa imani au jamii ya watu wengine linaweza kuwa tatizo kubwa huko mbele.
“Hakuna haja ya maigizo kuchafua watu wengine, heshima kwa wote ni jambo jema ambalo linaweza kuongeza upendo kwa kila jambo ufanyalo kwa jamii nyingine.
“Wakifanya kazi zao kwa ufasaha bado taifa litawaheshimu, hakuna mtu ama kundi ambao wangependelea kutokee vurugu eti kwa sababu ya maigizo ya mtu fulani, haiwezi kuungwa mkono,” alisema askofu huyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...