Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, February 2, 2014

TIMU YA NGUMI KIGOMA YATAMBA KUCHUKUA UBINGWAJUMA LESSO
KOCHA wa timu ya ngumi  Mkoa wa Kigoma Juma Lesso amesema timu yake ya mkoa imekuja kamili kwa ajili ya mashindano ya wazi yatakayofanyika Feb 5 

katika viwanja vya Tanganyika Pekazi vilivyopo kawe jijini Dar es salaam

ni mara ya kwanza kwa timu ya Mkoa wa Kigoma kushiriki mashindano makubwa kama haya timu hiyo ambayo imeweka kambi yake maeneo ya kawe kabla ya hapo ilikuwa maeneo ya mabibo na sasa kawe kwani mashindano hayo yalikuwa yafanyike Feb mosi mwaka huu na sasa ni feb 5

lakini tuna mshukulu sana Mkuu wa Mkoa wa Kigoma  Kanali Mstaafu Issa Machibya kuakikisha tunashiriki katika mashindano haya kwa mara ya kwanza 
timu hiyo ambayo imekuja na wachezaji kumi kati ya hawo wanawake watatu na wanaume saba ambao wakekuja kuwakilisha mkoa wa Kigoma tutahakikisha kuwa tunachukuwa ubingwa huo ambao upo wazi

Lesso ambaye ni kocha wa kimataifa wa mchezo huo ambapo amepitia kozi ya kimataifa ya mchezo huo Lesso aliwataja baadhi ya mabondia aliokuja nao kuwa ni Agnes Mushi, Ezira Josefu,Rashidi na Habasi na wengine ambao walikuwa katika kambi ya mkoa huu  wa Kigoma 
ambapo tumepewa sapoti kubwa sana na mkuu wa mkoa hivyo tutaakikisha atumwangushi na tunarudi na ubigwa kigoma kwani tumejipanga kwa ajili ya kuchukua nafasi ya juu kabisa kwani sasa ngumi Dar es salaam akuna tunahamishia mkoa wa kigoma ambapo amasa inaendelea hivyo tunawaomba wana Kigoma wote waliopo Dar watupe sapoti ili mambo yawe safi na mchezo wa ngumi uendelee kuwa juu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...