Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, July 6, 2013

Wateja Airtel sasa kujishindia Nyumba 3 za kisasa kupitia huduma ya YATOSHA


Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani)  nyumba watakayojishindia washindi wa Airtel Yatosha Shinda Nyumba 3 iliyozinduliwa leo  katika ofisi za Airtel Morrocco jijini Dar Es Salam ,akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel bi Anethy Muga
  Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani)  nyumba watakayojishindia washindi wa Airtel Yatosha Shinda Nyumba 3 iliyozinduliwa leo  katika ofisi za Airtel Morrocco jijini Dar Es Salam ,akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel , Anethy Muga.
*******

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania inayotoa huduma ya mawasiliano bora na nafuu zaidi nchini leo imezindua promosheni mpya kabambe itakayowawezesha wateja wote wa Airtel yatosha kujishindia zawadi mbalimbali huku wakiendelea kufurahia huduma ya Airtel yatosha ya siku, wiki au mwezi kama kawaida.

Uzinduzi wa promosheni hiyo mpya ya Airtel Yatosha inadhihirisha dhamira halisi ya Airtel kupitia huduma yao kabambe ya Airtel Yatosha yenye lengo la kutoa huduma nafuu huku wakiendelea kuwafaidisha wateja
wao nchi nzima.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo katika ofisi kuu ya Airtel Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw, Suni Colaso alisema "Leo Airtel tunafanya tukio la kihistoria mara baada ya uzinduzi wa huduma ya Airtel yatosha.
Sasa tunawazawadia wateja wetu wa Yatosha kwa aina ya kipekee kabisa, Kila atakaejiunga na huduma ya Airtel Yatosha moja kwa moja atakuwa amejihakikishia nafasi ya kujishindia zawadi ya Nyumba ya kisasa au kitita cha Pesa taslim.  Tutakuwa na mshindi mmoja wa kila siku atakaeibuka na shilingi milioni moja, na kama hiyo haitoshi kila mwisho wa mwezi tutatoa nyumba moja kwa mshindi mmoja kwa muda wa miezi mitatu"

Nyumba tunazotoa kwa wateja wetu ni za kisasa kabisa ili kudhihirisha  uwa Airtel Yatosha, ni nyumba yenye vyumba vitatu, sebule pamoja na jiko, itakuwa ndani ya fance iliyonakishiwa katika hali ya mvuto zaidi ili kumfanya mshindi wetu kufurahia zaidi kuwa mteja wa Airtel yatosha", aliongeza kusema Bw Colaso

Akifafanua jinsi ya kushiriki promosheni hiyo Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga alisema  " Ili mteja kushiriki promosheni hii, mteja atatakiwa kuendelea kujiunga na kutumia huduma yetu ya Airtel Yatosha ya Kila IKU, WIKI, au MWEZI kwa kupiga *149*99#,  kwa kufanya hivyo moja kwa moja utakuwa umeingia kwenye nafasi ya droo ya kila siku, wiki  au ya mwezi na unaweza kujishindia zawadi zetu kabambe Ikiwemo Nyumba.

Promosheni hii ya Airtel Yatosha ni maalum kwa wateja wote wa Airtel
yatosha wa malipo ya kabla, Ikiwa hujajiunga na Airtel jiunge leo na utumie huduma ya Airtel Yatosha ili upate nafasi ya kujishindia nyumba ya kisasa kila mwisho wa mwezi au pesa taslimu ndani ya siku tisini kila siku

Airtel ilizindua huduma ya Airtel Yatosha miezi mitatu iliyopita kwa lengo la kuwawezesha wateja wake kupata huduma bora na nafuu zaidi, lengo la huduma hii ni kumpatia mteja huduma nafuu ya sms , muda wa maongezi pamoja na kufurahia mtandao wa interneti wa 3.75G kwa masaa 25 tangu kujiunga.  Kujiunga mteja anatakiwa kupiga *149*99# na kujichagulia kifurushi kinachomfaa kwa SIKU, WIKI au MWEZI.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...