Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 5, 2013

MSECHU: VIDEO YA 'kIBUDU' NITAIFANYA KENYA



 Na Elizabeth John



HATIMAYE ngoma inayokwenda kwa jina la ‘Kibudu’ liyoimbwa na mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Peter Msechu, imeanza kutamba katika vituo mbalimbali vya redio kutokana na ujumbe wa mashairi yaliyomo ndani yake.

Mbali ya kutamba na kibao hicho, mkali huyo alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Relax’, ‘Kumbe’ ambavyo vilifanya vizuri zaidi mbali na kuwa na vibao vingi ambavyo vilimtambulisha katika tasnia ya muziki huo.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Msechu alisema katika kazi hiyo kamshirikisha mkali wa muziki huo, Ally Nipishe na kwamba tayari imeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Alisema kibao hicho kakitengeneza katika studio ya Ufundi Production chini ya mtayarishaji wake mahiri, Fundi Samuel.
“Naomba mashabiki wangu wakipokee vizuri kibao hicho ambacho natarajia kukifanyia video yake Nairobi, Kenya,” alisema.


Msechu aliwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa ajili ya video hiyo ambayo anatarajia kuitoa mwinzoni mwa mwezi ujao ikiwa ni pamoja na nyimbo nyingine nyingi zinazofuata.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...