Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, March 5, 2014

WAUGUZI NA MADAKTARI WASITISHA KUTOA HUDUMA KWA WAGONJWA BAADA YA HOSPITALI KUKUMBWA NA MAFURIKO



 Huu ni mtaro wa kupitisha maji taka ambao umepita kati kati ya Hospitali ya Palestina amapo ulifumuka na kusababisha kusambaa kwa maji machafu katika kila kona ya Hospitali hiyo
 Mmoja wa wagonjwa akiwa anangojea kupata huduma baada ya mvua hiyo kubwa kwisha
 Haya ni maji machafu ambayo yametapakaa kila sehemu ya hospitali
 Kushoto ni Mgonjwa akiwa amelala juu ya Benchi ambapo pembeni kuna maji na matope ambayo yamechanganyikana na kinyesi kutoka katika vyoo mbalimbali katika makazi ya watu.
 Hii ndio hali halisi ya Chemba hii ambayo ipo ndani ya Hospitali ya  Sinza Palestina
 Hizi ni chemba zaidi ambazo zipo nje na pia zimeungana na zilizopo ndani ya Hospital hiyo
 Wagonjwa zaidi wakingojea waganga kufika pia kumalizia kusafishwa kwa vyumba hivyo ili wapate hudumiwa
 Moja ya Chumba ambacho kilikuwa kimejaa tope kikingojea kusafishwa
 Hapa hata hapapitiki
 Baadhi ya viti vikiwa vimeegeshwa kwa ajili ya kungoja kufanya usafi
 Hakuna mtu katika maeneo haya kutokana na mvua kubwa iliyonyesha
 Kila kitu kimekaa hovyo hovyo baada ya mvua kubwa hiyo kunyesha
 Baadhi ya vifaa vya kutibia wagonjwa vikiwa juu ya moja ya kitanda cha kutibia wagonjwa huku watu wakingoja huduma ya matibabu.
 Huu ndio Mtaro wa maji machafu ambapo maji kutoka nje yamepita ndani ya hospitali hiyo na kusababisha maafa baada ya Mtaro huo kuziba.

Mapema mchana wa leo kumetokea mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es salaam kumesababisha usumbufu mkubwa baada ya maeneo mengi kukumbwa na tatizo la maji mengi ambayo yaliziba barabara , nyumba za watu pamoja na maeneo mbalimbali.

Mvua hizo kubwa ambazo hata mamlaka ya hali ya hewa wametahadhalisha kwamba zitakuwepo kuanzia Tarehe 5.03.2014 hadi Tarehe 7.03.2014  zimesababisha usumbufu mkubwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Kinondoni Sinza - Palestina kujaa maji kila kona na kupelekea wauguzi kuacha kazi na kupanda juu ya Meza na viti wakikwepa maji hayo. Na wengine kukimbia katika eneo hilo kuhofia maji hayo.

Walikwepa maji hayo kutokana na kwamba si ya mvua tuu lakini yalikuwa ni Machafu yaliyochanganyikana na maji kutoka vyooni ambapo kuna chemba moja ya maji machafu imepita hapo.

Baada ya mvua hiyo kwisha iliwalazimu wafanya usafi wachukue muda wa zaidi ya dakika 30 kufanya usafi na kutoa matope yaliyokuwa yamejaa kila chumba.
Akiongea kwa Simu Mganga Mkuu wa Hospitalu hiyo amekili kwamba kuna usumbufu mkubwa wa chemba hiyo na mvua hasa katika kipindi hicho ambapo zinanyesha kwa kiasi kikubwa. 

Ameongeza kwa kusema kwamba kunajuhudi zinahitajika kufanyika ili kuweza kunusuru tatizo hilo lisiendelee.
Nao baadhi ya wagonjwa ambao wengine walikuwa katika hali ambayo si nzuri wamesema  wanaiomba serikali itazame tatizo hilo maana licha ya maji hayo kuwa mengi lakini pia ni hatari kwa afya zao kwa ujumla.

Hii ndio picha halisi ilivyokuwa katika picha hizi..
Picha zote na Dar es salaam yetu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...